December 24, 2014

MAKAMU MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA AKUTANA NA VIONGOZI WA WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO DAR

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Taifa Ndugu Mboni Mhita Ambaye Pia ni Katibu Mkuu wa Pan African Union Ulio Chini ya Umoja wa Afrika AU  Anayehusika Kushugulikia Ajira kwa Vijana, Fursa, Elimu Afya na Mambo yanayuwahusu Vijana Akiwasikiliza Kwa Makini Viongozi wa Mtandao wa wafanyabiashara Ndogondogo Kutoka Mkoani Dar Es salaam Aliokutana nao Leo Kusikiliza Changamoto zinazowakabili Vijana hasa Wafanyabiashara Ndogondogo  Maarufu Kama wamachinga waliopambana na Jeshi la polisi jana.

Katika Kiako Hicho Viongozi wa wafanyabiashara Ndogondogo wameeleza Changamoto zinazowakabili kama Ukosefu wa Maeneo ya Kufanyia Biashara ,Kutokutambuliwa na Idara Yoyote ya serikali na Kutokusajiliwa .

Mhita  Amezichukua changamoto hizo kwenda kujadiliana na wadau mbalimbali kuona namna ya kuzitatua ili Wafanyabiashara hao waweze kufanya biashara kwa uhuru na haki bila kubugudhiwa na watendaji  wachache wanaowatumia wafanyabiashara hao kwa maslai yao binafsi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa wafanyabiashara Ndogondogo Kutoka Mkoa wa Dar es salaam Ndugu Job Mwakatobe Akimweleza Ndugu Mhita Changamoto Kubwa Zinazowakabili wafanyabishara ha.
 Viongozi wanaounda Mtandao wa Umoja wa wafanyabiashara Ndogongodo wakijadiliana Jambo katika Kiakoa hicho.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Taifa, Ndugu Mboni Mhita  Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Viongozi hao leo.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Taifa Ndugu Mboni Mhita  Akiwa na Viongozi wa Mtandao wa wafanyabiashara Ndogondogo Mkoani Dar es Salaam wakiwa Eneo la machinga Complex Kujionea hali hali mara baada ya Viongozi hao kumweleza ya kumwa Eneo Hilo lilijengwa Maalum kwajili ya wamachinga lakini cha kushangaza Wamepangishwa wafanyabiashara Wakubwa na Maofisi 
Ndugu Mboni Mhita Akizungumza na Wafanyabiashara Ndogondogo aliotembelea Eneao hilo na kukuta Sehemu Kubwa Ikiwa Haina watu
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Taifa Ndugu Mboni Mhita  Akishuhudia Jengo Malum la Wafanyabiashara Ndogondogo la Machinga Complex likiwa Tupu wakati wafanyabiashara hao hawana Maeneo ya Kufanyiabishara ikielezwa Kwamba chanzo cha Jengo Hilo kuwa wazi ni Urasimu wa Namna ya Kupata eneo la Kufanyia Biashara

Maeneo ya wamachinga  Ilala
Ndugu Mboni Mhita akiangalia bidhaa za machinga

Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa CCM Taifa Ndugu Mboni Mhita  Akiagana na Viongozi wao wakipeana Mkakati wa namna ya Kutatua Changamoto zinazowakabili.

No comments:

Post a Comment