Kundi zima la Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi,
litafanya utambulisho wa wimbo wao mpya “Sura Surambi” kwa wakazi wa Morogogo
Disemba 25 kwenye maadhimisho ya siku ya Christmas.
Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Ramadhani maarufu
kama Isha Mashauzi (pichani juu), ameuambia mtandao huu
kuwa onyesho hilo litafanyika ndani ya ukumbi wa Savoy Hotel na watasindikizwa
na mfalme wa kigodoro Msaga sumu.
Isha amesema “Sura Surambi” ni ngoma yao mpya kabisa
iliyoachiwa mwishoni mwa mwezi uliopita na Morogoro unakuwa ndio mji wa kwanza
baada ya Dar es Salaam, kuonjeshwa ladha ya wimbo huo ambao unafanya vizuri
sana kwenye vituo vya radio.
“Huu ni utunzi na uimbaji wangu mimi mwenyewe, sina mengi
ya kuongea zaidi ya kuwaahidi wakazi wa Morogoro burudani iliyokwenda shule,”
alisema Isha.
Sura Surambi ni maandalizi ya albam mpya ijayo ya
Mashauzi Classic ambapo tayari nyimbo mbili zimesharekodiwa, hii ikiwa ni
pamoja na “Ubaya Haulipizwi” ulioimbwa na Asia Mzinga, binti wa waimbaji
wakongwe wa taarab Abbas Mzinga na Bi Mwanamtama Amir.
No comments:
Post a Comment