La Veda akipozi na baadhi ya wadau waliofika kumpokea.
MWANADADA,
aliyeiwakilisha Tanzania katika shindano la Big Brother Hotshots, Irene
Neema Vedastous ‘LA VEDA' amefunguka kuwa Diamond, Fezza na Idris
wameondoa gundu kwa ushindi wao.
Akizungumza
na GPL jana jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, wakati akiwasili kutoka Afrika ya Kusini alipokwenda kuungana
na washiriki wengine wa BBA katika fainali, La Veda alisema,
“Binafsi
nimefurahi sana kwa Idris kushinda Dola za Kimarekani 300,000, ni
furaha kubwa sana kwangu na kwa Watanzania kwani naamini pia Diamond
kuchukua tuzo tatu za Channel O na nyingine aliyopata juzi kutoka
Nigeria, Fezza kuingia tena mjengoni wote watakuwa wameondoa gundu kwa
wasanii wa Kitanzania’, alisema.
Aidha
La veda amewaomba Watanzani kujitokeza kwa wingi kumpokea Idris siku
atakapowasili maana ushindi wake unazidi kuiweka Tanzania katika ramani
nzuri kimataifa.
No comments:
Post a Comment