December 09, 2014

KONGAMANO LA SIKU MBILI VITA DHIDI YA UKATILI KWA WANAWAKE NA WALEMAVU LAFANYIKA MKOANI MOROGORO

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani akihutubia wakati akifungua Kongamano la Majadiliano kuhusiana na vitendo vya ukatili kwa wanawake na walemavu Mkoani Morogoro leo. Kongamano hilo ambalo limeshirikisha wadau mbalimbali kutoka baadhi ya mikoa ya Tanzania limeandaliwa na Shirika la Seed Trust la mjini Morogoro kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA). Kulia ni Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mary Massay na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Seed Trust, Margareth Mkanga (MB).
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Seed Trust, Margareth Mkanga (MB). Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani na Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mary Massay.
 Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mary Massay (katikati),akihutubia katika kongamano hilo. Kulia ni Mwakirishi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya idadi ya watu Duniani (UNPFA), Anna Holmstrom na  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Seed Trust, Margareth Mkanga (MB).
 Mwakirishi wa Shirika la Kimataifa linaloshughulikia masuala ya idadi ya watu Duniani (UNPFA), Anna Holmstrom, akitoa hutuba yake kwenye kongamano hilo.
 Ofisa Mipango wa Shirika la Afya Dunia Duniani (HWO) Tanzania, Dk.Theopista John Kabuteni, akisoma hutuba katika kongamano hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Seed Trust, Stephen Mashishanga akitoa maagizo ya kushughulikia suala na mtoto kubakwa na mtuhumiwa kuwa huru mtaani.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomelo, Anthony Mtaba akizungumza katika kongamano hilo. Kulia ni Ofisa Tarafa wa Manispaa ya Morogoro, Mlange Pakalapakala Jumamosi na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Gemini Mushi.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk.Mtei akitoa ufafanuzi wa masula kadhaa.
Mratibu wa Kongamano hilo, Peter Mwita akizungumza na washiriki kuhusu masuala mbalimbali.
Viongozi mbalimbali wakiwa meza kuu.
Washiriki wa semina hiyo wakiimba wimbo wa taifa.
Washiriki wakiwa kwenye semina hiyo.
Kongamano linaendelea.

Bodi ya Shirika la Seed Trust katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa.
*****
Dotto Mwaibale, Morogoro
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani amesema kila mtu kwa nafasi aliyonayo ana wajibu wa kupinga vitendo vya ukatili kwa wanawake na walemavu.

Katika hatua nyingine amewataka mahakimu  nchini kuweka kipaumbele katika kesi za ukatili wa kijinsia zinazofika katika mahakama zao hili kutenda haki wakati wa kusikiliza mashauri mbalimbali.

Kombani alisema hayo Mkoani Mrogoro wakati akifungua  mkutano wa ukatili wa kijinsia kwa wanawake na walemavu ulioandaliwa na Shirika la  Seed Trust la mjini huomo kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa ambalo linashughulikia idadi ya watu Duniani UNFPA .

“Kila mtu anawajibu wa kuvipinga vitendo hivyo kwani wanaoathiriwa ni kila mmoja ndani ya familia" alisema Kombani.

Alisema kuwa vyombo vya kutoa haki kama mhakama kupitia kwa Mahakimu ni vizuri waweke kipaumbele cha kusikiliza kesi hizo haraka badala ya kuziche jambo litakalosaidia kuwabana watuhumiwa wa vitendo hivyo.

Alisema wahanga wakubwa wa vitendo hivyo ni watoto na wakinamama na baadhi ya wahusika ni jamii inayowazunguka pamoja na ndugu wa karibu.

Aliongeza kuwa Serikali ipo tayari kufanyia kazi matatizo yote ya kijinsia yanayo ibuliwa na wananchi , vyombo vya habari na tasisi binafsi ambazo zipo katika mapambano makubwa juu ya swala hili mtambuka.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tasisi isiyo ya kiserikali , Magreth Mkanga (MB), Alisema kuna haja ya kila mtu kuwa mlinzi wa mwenzie juu ya uakatili wa kijinsia na kuzifanya siku 365 kuwa ni siku za kupambana na ukatili huo kuliko hivi sasa ambao watu wameamua kutenga siku chache tu kwa mwaka.

Alitoa wito kwa wadau mbalimbali kuacha kufumbia macho maswala mbalimbali yanayojitokeza  katika jamii zinazotuzunguka.
(Imeandaliwa na mtandao wa habari za jamii.com)

No comments:

Post a Comment