Kocha maarufu nchini, Abdallah
‘King’ Kibadeni amezushiwa kifo na kusababisha utata mkubwa.
Taarifa ziliripotiwa na
mtandao mmoja zimefanya watu waanze kumpigia simu kila mara.
“Kweli hata mimi napigiwa simu
na watu wengi sana kama nimefariki dunia, hawa watu sijui wamepata wapi hizi
taarifa.
“Kweli siku chache zilizopita
nimefanyiwa upasuaji wa jicho. Hadi sasa niko safi kabisa, ninaendesha hata
gari.
“Kupitia mtandao wako, naomba
niseme hivi; ninawaomba radhi wote waliopata usumbufu kutokana na taarifa
hizi,” alisema Kibadeni na kuongeza.
“Ila ninaomba wale ambao wanaopata taarifa ni vizuri kuzihakikisha kuliko kusababisha usumbufu kwa watu.SALEHE JEMBE BLOG
No comments:
Post a Comment