December 06, 2014

EMERSON WA YANGA YULEEEE JUKWAANI

Siku chache baada ya kuwasili nchini kwa Mchezaji kutoka Brazili,Emerson de Oliveira Neves Roque aliyekuja nchini kyufanya majaribio ya kusakata kabumbu na wakali wa mtaa wa Jangwani Yanga Afrika, mtandao huu wa Father Kidevu Blog ulipekenyua na kurusha habari kuwa Emerson katika timu yake iliyomsajili hakuwahi kucheza mchezo hata mmoja na hata kuonekana katika orodha ya wachezaji wa akiba ilibezwa na baadhi ya mashabiki na wapenzi wa Yanga. 

Lakini lililoandikwa na FK Blog limejidhihirisha hii leo kufuatia Mrazili, Marcio Maximo anaekinoa kikosi hicho cha mabingwa wa mara 24 wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara kuto mpanga mchezaji katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Express FC ya Uganda. 

Emerson alionekana jukwaani katika jukwaa la Orange akiwa anapiga picha za aina mbalimbali na mashabiki na wapenzi wa timu ya Yanga jambo ambalo baadhi ya mashabiki wakiwa wameduwaza na uamuzi wa maximo kumuweka benchi kiungo huyo licha ya kumpa mkataba wa mwaka mmoja kusuguma gozi la ngombe Jangwani.

Kiungo huyo kutoka timu ya Bonsucesso FC inayoshika nafasi ya 13 na imeshinda michezo mitatu na kupoteza michezo 6 na kutoka suluhu michezo 6, alikuwa jukwaani akiwa amevalia kaptura yake ya jinsi na car wash ya kijivu huku masikioni akiwa na hereni za silva kadhalika puani ana kishaufu.
 
Yanga inataraji kushuka dimba la Uwanja wa Taifa jumamosi a Desemba 13 mwaka huu katika mchezo wa Nani mtani Jembe ambapo mashabiki wa Yanga wanataka kumuona Kiungo wao huyo mpya akicheza samba la kibrazili. 
 Lineup ya leo ya Yanga.
 
Baada ya kupiga sana picha na mashabiki sasa Emerson alikuwa akijiangalia kucha...

No comments:

Post a Comment