Rais Jakaya Kikwete, akiteta jambo na Mwenyekiti wa
Chadema, Freeman Mbowe (kushoto) na Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakati wakiwa katika
maziko ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia
juzi.
Rais Jakaya Kikwete, akisaini katika kitabu cha
maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan
Bwanamdogo, aliyefariki dunia juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika
kijijini kwake Chalinze Miono, Wilaya ya Bagamoyo
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal, wakiwaongoza waombolezaji kuswalia mwili wa marehemu Ramadhan
Bwanamdogo, aliyekuwa Mbunge wa Chalinze, aliyefariki juzi. Mazishi ya mbunge
huyo yamefanyika leo kijijini kwao Miono.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, akisaini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa
Mbunge wa Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ramadhan Bwanamdogo, aliyefariki dunia
juzi. Maziko ya marehemu Bwanamdogo, yamefanyika kijijini kwake Chalinze Miono,
Wilaya ya Bagamoyo.
No comments:
Post a Comment