Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako
Manongi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya mwaka 2013 ambayo
hutolewa kila mwaka na Shirika la Afya Duniani, Balozi aliwaeleza
wageni waalikwa katika hafla hiyo kwamba ushiriki wa viongozi wa afrika
kupitia mtandao wao wa ALMA umechangia sana katika kupunguza idadi ya
vifo vitokanavyo na Malaria
Dkt. Robert Newman kutoka WHO yeye amesema, inasikitisha pale
inapobidi mtoto apoteze maisha kwa sababu tu ameshindwa kupatiwa
chandarua ambayo thamani yake ni dola tano. amewataka viongozi na
washirika mbalimbali kutobweteka na mafanikio katika kuudhibiti ugonjwa
huo mafanikio nayohusu kupungua kwa maambukizo ya ugonjwa wa malaria
na vifo vya watoto chini ya miaka mitano.
Bw, Ray Chambers ambaye ni Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, amesema inatia moyo sana kuona vitanda katika wadi za watoto
vikiwa vitupu mahali ambapo watoto walikuwa wakilala wawili katika
kitanda kimoja kutokana na kusumbuliwa na malaria.
Dkt. Fatoumata Traore ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa Roll Back Maralia akizungumza wakati wa halfa hiyo.
Katibu Mtendaji wa ALMA Bi. Joy Phumapi naye akizungumza machache
*********
Na Mwandishi Maalum
Utashi wa kisiasa unaoonyeshwa na marais wa Afrika katika kudhibiti ugonjwa wa malaria, pamoja
na ushiriki wa wadau mbalimbali akiwamo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon
umeanza kuzaa matunda kufuatia
taarifa za kutia matumaini zinazoonyesha kupungua kwa vifo vitokanavyo na ugonjwa wa
malaria.
Akizungumza wakati wa uzinduzi
wa ripoti ya mwaka 2013 ya Shirika la
Afya la Dunia ( WHO ) kuhusu mwelekeo wa ugonjwa wa malaria katika kipindi hicho , Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania
katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako
Manongi amesema hapana shaka kwamba mwamko
ulioonyeshwa na Marais wa Afrika kupitia muungano wao dhidi ya Malaria ( ALMA) umechangia kwa kiasi kikubwa.
Jana Alhamis
Bw. Ray Chambers ambaye ni mjumbe maalum wa katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa kuhusu Malaria kwa pamoja na Dkt.
Robert Newman ambaye ni Mkurugenzi wa
mradi wa Malaria (WHO), Bi. Fatoumata
Traore Mkurugenzi Mtendaji wa Roll Back Malaria na Bi. Joy Phumapi ambaye ni Katibu Mtendaji wa ALMA
walizindua ripoti hiyo mbele ya Wawakilishi wa Kudumu wa Nchi za Afrika na
wadau wadau wengine.
Akiwakaribisha wageni waalikwa
kwa niaba ya Balozi wa Msumbiji katika
hafla hiyo iliyoandaliwa na ALMA, Balozi Manongi alisema ripoti za kila mwaka za WHO zimekuwa
zikionyesha mwelekeo mzuri katika
kuushughulikia ugonjwa huo ambao
unaadhiri kwa kiasi kikubwa watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano.
Na kusisitiza kwamba Afrika inatakiwa kuzitumia ripoti hizo kuongeza kasi
katika kuikabili Malaria.
“Ripoti hizi zinaonyesha
kwamba tukishirikiana tunaweza kabisa kuidhibiti malaria, viongozi wetu
wameonyesha mfano kwa kuanzisha muungano wao dhidi ya malaria, ni wajibu wetu kuendelea
kukusanya nguvu na kujituma Zaidi ili tusirudi nyuma” akasisitiza Balozi
Manongi.
Ripoti ya malaria kwa mwaka
huu, ambayo ni mkusanyiko wa taarifa kutoka nchi 102 zikiwamo 10 ambazo zimeathirika sana na ugonjwa wa
malaria na taarifa kutoka vyanzo vingine, inatoa tathmini ambayo pamoja na mambo mengi kwamba onyesha ushirikiano kati ya serikali, mashirika ya
kimataifa na wafadhili umewezesha katika kipindi cha mwaka 2000-2012 kuokoa
maisha ya watu 3.3 milioni ambayo yangepotea kutoka na ugonjwa
huo.
Taarifa hiyo inaeleza Zaidi kwamba ugonjwa wa malaria umepungua kwa asilimia 45 duniani kote na kwa asilimia 49 katika nchi
za Afrika zinazohudumiwa na WHO.
Akizungumza katika uzinduzi
huo Dkt. Robert Newman kutoka WHO
amewaeleza Mabalozi kwamba ripoti inahabari njema kuwa ugonjwa wa malaria
umepungua kwa kiasi kikubwa sana katika kipindi hicho cha kati ya 2000-2012
“ kuna punguzo la asilimia 54
la vifo vya watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano vitokanavyo na malaria
katika nchi za afrika hususani zile
ambazo zimeathirika Zaidi. Takwimu hizi
na nyingine zilizomo katika ripoti hii
zinathihirisha wazi kwamba
tukishirikiana tunaweza kuleta mabadiliko makubwa katika kuikabili
Malaria” akasema Dkt Newman
Akaongeza kwamba licha
utashi wa kisiasa ulioonyeshwa na viongozi mbalimbali kumekuwapo na mwitikio
unaoridhisha wa uchangiaji wa raslimali fedha katika eneo hilo. Ambapo katika
kipindi hicho jumla ya dola za kimarekani bilioni mbili zilitolewa na
wafadhili na dola milioni mia
tano zilitolewa na nchi ambazo
zimeathirika Zaidi.
Hata hivyo akasema ingawa mwamko wa kuchangia umekuwa mkubwa bado lengo halijafikiwa la kiasi cha dola za
kimarekani 5.1 na kuonya kwamba bado
michango inahitaji na wala mafanikio hayo yaliyopatikana
yasijewafanya wadau wakabweteka kuchangia au kuhamishia fedha kwenye masuala mengine.
“ hatupashwi kubweteka au
kuridhika na mafanikio haya, haipendezi mtoto au mtu kufariki kwa sababu tu ya
kushindwa kuwa na uwezo wa kununua
chandarua ambayo thamani yake ni sawa na dola tano ya kimarekani. Na weza kusema mafaniko haya ni sawa na nusu glasi.
Hebu pata picha kama wewe ungekuwa ni
mtoto unayeishi katika maeneo ambayo yameathirika vibaya na malaria halafu
hakuna hata dawa za kukutibu, bila shaka matarajio yako ni kuona glasi imejaa na
si nusu glasi au glasi iliyotupu” akasisitiza Muwakilishi huyo wa WHO.
Naye Mjumbe
Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu
Malaria na ambaye amekuwa mstari
wa mbele katika kuchagiza na kutafuta
raslimali zikiwamo fedha kwaajili ya miradi ya malaria, Bw. Ray Chambers
alikuwa na haya ya kusema
“Ripoti hii ya WHO inatoa matumaini sana, ukizingatia kwamba katika miaka
iliyopita takribani watoto milioni
moja walikuwa wakipoteza maisha kwa
malaria leo hii idadi hiyo imepungua hadi kufika nusu ni jambo la
kutia faraja sana” akasema Chembers
Na kuongeza. “ nimetumia muda mwingi Afrika
nimeshuhudia watoto wakifariki,
nimejionea wadi za watoto
zilivyokuwa zimejaa huku watoto wakilala wawili katika kitanda kimoja. Lakini
leo hii katika baadhi ya nchi wadi za watoto zipo tupu na vitanda vinatumika
kwa huduma nyingine”.
No comments:
Post a Comment