December 13, 2013

MTEMVU AZIDI KUWAPATIA WATANZANIA KAZI DUBAI

 Mwenyekiti wa Kampuni ya Bravo, Abbas Mtemvu (kulia) akimkabidhi Mkazi wa Bagamoyo, Asha Vitalis tiketi ya ndege na nyaraka zingine kwa jili ya safari ya kwenda kufanya kazi Dubai, aliyotafutiwa kazi na kampuni hiyo. Hafla hiyo ya kukabidhi tiketi kwa Watanzania wawili walioondoka  kwenda kufanya kazi Dubai, ilifanyika Dar es Salaam juzi. Mpaka sasa kampuni hiyo imewatafutia kazi ughaibuni zaidi ya Watanzania 100.
 Mwenyekiti wa Kampuni ya Bravo, Abbas Mtemvu (kulia) akimkabidhi Mkazi wa Kinondoni, Neema Ndunguru tiketi ya ndege na nyaraka zingine kwa ajili ya safari ya kwenda kufanya kazi Dubai, aliyotafutiwa na kampuni hiyo. Hafla hiyo ya kukabidhi tiketi kwa Watanzania wawili akiwemo Asha Vitalis (aliyekaa kushoto) walioondoka  jana kwenda kufanya kazi Dubai, ilifanyika Dar es Salaam juzi. Mpaka sasa kampuni hiyo imewatafutia kazi ughaibuni zaidi ya Watanzania 100.
 Mtemvu akiwasihi Asha na Neema kulinda maadili na heshima ya Tanzania wakiwa kazini
 Asha na Neema wakisikiliza kwa makini wakati Mtemvu alipokuwa akizungumza nao kuhusu ajira yao hiyo
 Mtemvu akiwa na Asha, Neema pamoja na baadhi ya wadhamini wao na baadhi ya maofisa wa Kampuni ya Bravo.
Mtemvu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, Dar es Salaam, akiwa katika picha ya pamoja na Asha (kushoto) na Neema baada ya kuwakabidhi tiketi.

No comments:

Post a Comment