December 16, 2013

UNIC YAFANYA MAFUNZO YENYE TIJA YA UJASIRIMALI PEMBA

DSC_0181
Mshehereshaji Bw. Salum Msellem kutoka Istiqama Radio akitambulisha meza kuu kwa washiriki wa mafunzo ya Ujasiriamali ya siku moja kwa Vijana Visiwani Pemba yaliyofanyika mwishoni mwa juma kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari Madungu.
DSC_0240
Mratibu wa YUNA kisiwani Pemba, Bw. Mohammed Ali, akisoma taarifa ya maendeleo ya vilabu vya Umoja wa Mataifa visiwani humo na changamoto zinazowakabili kwa walezi wa vilabu hivyo.
.Vijana waaswa kujikita katika ujasirimali ili kuondokana na umaskini 

Na Mwandishi Wetu
Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), kilifanya mafunzo yenye tija ya ujasirimali kwa vijana katika Mji wa Pemba visiwani, Zanzibar na kupata washiriki wenye kiu ya kutaka kujiajiri na kuondokana na umasikini hapa nchini.

Akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa mafunzo hayo ya siku moja ya ujasirimali kwa vijana hivi karibuni Mjini Pemba, Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama amesema Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2000 walizindua malengo ya milenia ili kusaidia nchi zinazoendelea kuondokana na umaskini.

“malengo manane ya milenia ni pamoja na Afya ya Uzazi kwa kinamama, Elimu, kuondoa umaskini na mambo ya mazingira vile vile kusaidia mikakati mbalimbali ya nchi hizo katika utekelezaji wake mpaka kufikia mwaka 2015,” amesema Bi. Ledama.
DSC_0265
Afisa Vijana - Mshauri kutoka WIZARA ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na Watoto, Bi. Stara Salim akizungumzia jitihadi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuwawezesha Vijana kupata mikopo kupitia asasi mbalimbali za fedha ili waweze kujikwamua kimaisha na kuondokana na lindi la umaskini visiwani Pemba.

Amesema kwamba kazi kuu ya Umoja wa Mataifa na taasisi zake ni kusaidia Serikali mbalimbali katika nchi zinazoendelea kufanikisha mikakati na utekelezeji wa malengo ya milenia ikiwemo dhana ya kupunguza umaskini.

Bi.Ledama alilisitiza kwamba katika utekelezaji huo Umoja wa Mataifa inasaidia mikakati hiyo ya kuondoa umaskini kwa kuandaa program mablimbali na kufanya mafunzo ya ujasirimali kwa vijana ili waweze kujiajiri na kuondokana na umasikini.

“Serikali pekee haiwezi kutoa ajira kwa watu wote kwa sababu nafasi ni chache na mahitaji ni makubwa kwa hiyo ndugu zangu kujiajiri na kuajiri wengine katika sekta binafsi kupitia ujasirimali ni nafasi pekee ya kuondokana na umaskini,” aliongeza.

Amesema kwamba asilimia 43 ya wakaazi wa Zanzibar ni vijana kwa hiyo kuna umuhimu mkubwa kwa Umoja wa Mataifa na sekta binafsi kuhamasisha ujasirimali kama njia pekee ya kujiajiri na kuondokana na umaskini wa kipato na wa jumla.
DSC_0278
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumzia lengo la kuendesha mafunzo ya Ujasiriamali kwa watu walio nje ya shule ikiwa ni moja ya agenda ya kutekeleza malengo ya milenia ya kupunguza umaskini kwa nchi zinazoendelea.

Bi. Ledama amesema sekta binafsi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wanaweza kupunguza tatizo la ajira kwa kusisitiza ujasirimali zaidi katika maeneo mbalimbali ya Bara na Visiwani.

“Haya ni mafunzo ya pili kufanyika bara na visiwani yenye kutoa mafunzo yenye tija juu ya ujasirimali na faida zake katika kupunguza na kupambana umasikini kwenye nchi zinazoendelea,” aliongeza.

Amesema kwamba Shirika la Kazi Duniani (ILO) wana kitengo maalum cha mambo kujenga uwezo kwa vijana na mafunzo ya ujasirimali yenye lengo la kuondoa umasikini miongoni mwa vijana nchini Tanzania.
DSC_0377
Mkufunzi wa mafunzo ya Ujasiriamali kupitia Program ya kazi Nje nje inayolenga kuelemisha Vijana stadi za Ujasiriamali iliyoasisiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) Bi. Mwanapili Hamad akitoa mada kuhusu dhana nzima ya uongozi katika biashara (Business Management) kwa wajasiriamali Vijana visiwani Pemba ili waweze kuboresha kipato chao.
DSC_0220
Picha juu na chini ni sehemu ya washiriki wa mafunzo ya Ujasiriamali ya siku moja yaliyoratibiwa na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).
DSC_0354 
DSC_0228
DSC_0466
Mjasiriamali mwenye kipaji cha kuchora ramani za majengo, kutengeneza sampuli za nyumba kwa kutumia maboksi Bw.Steven Timothy Mihale kutoka Temeke Youth Development Network (TEYODEN) akionyesha moja ya kazi zake kwa wajasiriamali wenzake ambayo inampatia kipato na kuweza kuendesha maisha yake.
Bw. Steven Mihale aliwapa moyo wajasiriamali wenzake na kuwataka kuwa na uthubutu na kutokata tamaa mapema.
DSC_0486
Vijana wajasiriamali wakiangalia kazi ya Mjasiriali mwenzao.
DSC_0388
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akiuliza swali kwa wakufunzi wa mafunzo ya Ujasiriamali yaliyoratibiwa na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).
DSC_0498
Mkufunzi wa mafunzo ya Ujasiriamali Bi. Mgeni Salum akitoa somo la namna ya kuhifadhi hesabu za mauzo na kujua kama biashara ina faida au hasara sanjari na kupata mikopo kupitia taasisi za kifedha.
DSC_0391
Mratibu wa YUNA kisiwani Pemba, Bw. Mohammed Ali akiteta jambo Mkutubi wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Harriet Macha (katikati) wakati wa mafunzo ya Ujasiriamali kwa vijana visiwani Pemba yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Sekondari Madungu.
DSC_0524
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Usia Nkhoma Ledama, akifunga mafunzo ya siku moja ya wajasiriamali Visiwani Pemba yaliyoratibiwa na kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC).

No comments:

Post a Comment