Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Azam Media,Yussuf Bahresa akikata utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa Televisheni yao ya Azam kwenye makao makuu
yao yaliopo Pugu Road,jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi
mtendaji wa Azamtv, bwana Yusuf Bakhresa akizungumza na waandishi wa habari leo.
Mkurugenzi
mtendaji wa Azamtv, bwana Yusuf Bakhresa akisalimiana na wasanii wakati
wa ufunguzi wa ofisi ya AZAMTV siku ya jumatatu tarehe 16 Desemba 2013.
********
AzamTV leo
imeanza kutoa huduma zake rasmi katika makao makuu yaliyopo barabara ya
Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Huduma za
matangazo ya AzamTV zilianza kupatikana hewani Kuanzia Ijumaa Desemba 6, 2013
kwa kuwawezesha wateja waliounganishwa kwenya kisimbuzi kungalia bure hadi hii
leo ambapo huduma kwa malipo inaanza rasmi kwa ada ya shilingi 12,500 kwa
mwezi.
Kwa kuanzia huduma ya AzamTV itahusisha
chaneli 50 zinazojumuisha chaneli maarufu za kimataifa, chaneli maarufu za
ndani na chaneli tatu maalumu za Azam ambazo ni:
Azam One –
burudani kwa familia kutoka Afrika, sehemu kubwa ya matangazo itakuwa kwa lugha
ya Kiswahili.
Azam Two –
vipindi maalum kutoka sehemu mbalimbali za dunia
SinemaZetu
– Chaneli maalumu kwa tamthilia za kitanzania kwa saa 24.
Kwa
pamoja, chaneli tajwa zitawapa wateja wigo mpana wa kufaidi matangazo bora ya
michezo, tamthilia, watoto na maisha.
Ofisi
ilifunguliwa rasmi na Bw. Yusuf Bakhresa: Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media
Ltd.
“Ofisi
hii ya makao makuu ambayo kwa hakika ni ya kuvutia ni kielelezo cha nia thabiti
ya Azam Media kufanya kazi kwa umakini katika shughuli ya utangazaji hapa
Tanzania. Dira yetu ni kutoa burudani ya kiwango cha juu kwa familia kwa bei
nafuu kote nchini, na baadaye kote barani Afrika. Hili ni jambo ambalo kila
mmoja hapa nchini anapaswa kujivunia.” Alisema Bakhresa
Rhys
Torrington: Afisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media Ltd alisema: “Naona faraja kubwa
kwamba leo hii AzamTV ipo sokoni kwa
ajili ya kila mtanzania. Tutahabarisha, kuelimisha na zaidi ya yote
tutaburudusha watu kote nchini. Huduma yetu inapatikana kwa watu wote – situ
katika ofisi hizi lakini pia kupitia mtandao wetu unaohusisha zaidi ya mawakala
50 katika kila mkoa. AzamTV ni ya kudumu”
Azam Media
pia inawekeza katika utayarishaji wa vipindi vipya kupitia kampuni yake tanzu,
Uhai Productions, kwa kushirikiana na watayarishaji wa vipindi wa hapa
Tanzania.
No comments:
Post a Comment