Na Andrew Chale.
DESEMBA 24 ‘kesho’ Jumanne kutakuwa hakutoshi ndani ya mgahawa
na ukumbi wa kisasa wa Nyumbani Lounge kwenye bonge la ‘Party’ ya kuzaliwa kwa
Mama Mitindo nchini Tanzania, Asia Idarous Khamsin, atakapokuwa akitimiza miaka
54.
Party hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na mastaa mbali mbali wakiwemo wa filamu, muziki, mitindo na wabunifu.
Akizungumza na
mtandao huu, Asia Idarous ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashion, na
muandaaji wa onyesho kubwa la Kila mwaka la Mavazi lijulikanalo kama … Usiku wa
Khanga za Kale, anasema kuwa tayari mandalizi yameshakamilika na wadau mbali
mbali wanatarajia kuhudhuria kwenye ‘party’ hiyo itakayokuwa ya aina yake.
“Kesho Desemba 24, Ni siku yangu ya kuzaliwa, Namshukuru
Mungu kwa neema zake kufika hadi leo hii kwa ulinzi na muongozo wake, leo hii mimi kufikia hapa na kutimiza miaka hii
54” alisema Asia Idarous.
Akitoa nasaha zake kwa wabunifu wa mitindo wanaochipukia
hapa nchini, Asia aliwataka wasivunjike moyo kwani kazi hiyo inahitaji
uvumilivu na maalifa. “Namshukuru Mungu kwa kufikia hapa leo hii na hakika
nitaendeleza fani hii pia nawaomba wabunifu na wanamitindo wanaochipukia kuwa
na hali ya ushirikiano, kusaidiana, kuchapa kazi na kuwa na ‘tojo’ safi” alisema Asia Idarous Khamsin.
Aidha, Asia Idarous alisema kuwa milango ipo wazi kwa
wabunifu wa mitindo kupata ushahuri wake kwa watakaotaka huku akiwaombea wafike
mbali katika kuendeleza gurudumu la mitindo hapa nchini.
No comments:
Post a Comment