Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa, tarehe 25
Desemba 2013 atajumuika na watoto yatima wa kituo cha Mgolole Orphanage
kilichopo Bigwa nje kidogo ya Mji wa Morogoro.
Mrembo huo ataungana na warembo wengine watatu, akiwemo Miss
Tanzania mshindi wa pili Latifa Mohamed, Miss Tanzania mshindi wa tano
Elizabeth Perrty, na Sabra Islam Miss Morogoro 2013 ambaye ndie atakae kuwa
mwenyeji wao wakati wote wakiwa mkoani hapo.
Ni kawaida kwa Mrembo wa Taifa, Miss Tanzania kila mwishoni
mwa mwaka kula X Mass na Watoto Yatima, wasiojiweza pamoja na wale waishio
katika mazingira magumu.
Baada ya shughuli hiyo Miss Tanzania Happiness Watimanywa
atajumuika pia na watoto wa aina hiyo jijini D’salaam siku ya Mwaka mpya tarehe
1 January 2014 katika vituo vingine atakavyopangiwa na Kamati ya Miss Tanzania.
Pamoja na shughuli hiyo, Mrembo Happiness Watimanywa pia
anakusudia kusaidia jamii wenye matatizo
ya Maji kwa kuwachimbia visima vya maji safi katika mikoa ya Dodoma na Singida.
Miss Tanzania Happiness Watimanywa ambaye pia ni Miss Dodoma
na Miss Kanda ya Kati 2013, ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu nchini
Scotland ameahirisha masomo yake kwa muda wa mwaka mmoja hadi hapo atakapovua
Taji la Mrembo wa Taifa mwishoni mwa mwaka ujao 2014.
No comments:
Post a Comment