KANISA la
Katoliki, jimbo kuu la Arusha,jana limetoa tamko la kuitaka serikali
iseme ni kina nani wamehusika na tukio la kigaidi la kushambulia kanisa
lake la parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi la Olasiti huku,
likiwataka waumini wa kanisa hilo,kutolipiza kisasi na wawe tayari
kushinda ubaya kwa wema.
Katika tukio hilo
hadi jana mchana watu wawili na wengine 66 walikuwa wamejeruhiwa na
kati ya wanne bado hali zao ni mbaya huku huku wengine 34 wakiendelea na
matibabu hospitali ya Mount meru.
Waliofariki
ni Regina Saning’o Losyoki ambaye umri wake haujalikana aliyekuwa
muimbaji wa kwaya ya kanisa hilo na James Gabriel (16) ambaye alifia
Uwanja wa Ndege akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Muhimbili .
Askofu Mkuu wa
Jimbo Kuu Katoliki Arusha , Josephat Lebulu alitoa tamko hilo,
janawakazi akizungumza na waandishi wa habari, akiwa na Balozi wa
Vatcan nchini Tanzania, Askofu Mkuu Fransisco Padilla baada ya
kuwatembelea majeruhi wa tukio hilo lililotokea juzi.
“Msimamo wa
Kanisa katika hili, ni kuwataka waumini wasilipize kisasi kama ambavyo
alisema Yesu kristo kuwa Msilipize kisasi muwe tayari kushinda ubaya jwa
wema”alisena Askofu Lebulu,
Alisema maandikio
mara zote yanaelekeza kuwa na moyo wa kusamehe lakini pia Serikali
inapaswa kuchukuwa hatua kwa wahusika wa maovu.
Hata hivyo alisema lazima serikali iwaambie kina nani wamehusika na watachukuliwa hatua gani.
“tunataka mahakama zitowe maamuzi sahihi na pia serikali ipambane kuondoa mizizi ya ugaidi”alisema Lebolu.
Alisema kanisa linaamini kuwa waliotekeleza shambulio hilo, walifanyakazi ya shetani na sio ya waumini wa dini.
Akizungumzia ushauri wa kuongeza ulinzi katika makanisa na maeneo
mengine ya Ibada nchini, Askofu Lebulu alisema, kama mioyo ya watu
imeoza hata ulinzi ukiwepo matukio ya kigaidi yatakuwepo.
“tunapaswa kujiuliza ni kwanini haya yanafanyika sasa…ingekuwa
shambulizi hili limefanywa na mwizi basi tungesema tuongeze ulinzi
lakini hapa ndani ya mioyo ya watu kuna uovu na serikali inapaswa
kuondoa mizizi ya ugaidi”alisema Lebolu.
Askofu Lebulu
alisema baada ya tukio hilo, wamepokea pole kutoka nchi mbali mbali
duniani, ikiwepo Marekani, Italia,India na nyinginezo.
Awali kabla ya kutoa tamko hilo, Balozi wa Vatican Askofu Padilla
alitembelea majeruhi katika hospitali ya mkoa wa Mount Meru na kuwapa
pole kisha akawaombea ewapone haraka.
Hata hivyo, licha ya kulaani tukio hilo ambalo alisema ni baya, Balozi
huyo wa Vatican hakuwa tayari kuelezea zaidi hatua ambazo wanaweza
kuchukuwa kama Kanisa.
Askofu Lebulu asimilia kilichotokea kwa Makamu wa Rais
Askofu
Lebulu alisema juzi kabla ya kushambuliwa kanisani, walikuwa ndio
wanaanza ibada na hawakujua kilichotokea na alipogeuka yeye na balozi
waliona watu wakiwa wamelala chini huku wengine wakilia na kuumia sehemu
mbalimbali.
"Hii inasikitisha
na watanzania tujiulize kwanini hivi sasa watu wanauwa kama mbwa na
kwanini matukio haya yanajitokeza”alisema Askofu Lebulu.
Alisema hajuwi nia ya mhusika aliyelipua bomu alikuwa akimlenga nani
kama ni yeye au balozi na kama si balozi basi huyo mhusika ndio anajua.
“
naskia uchungu sana kwani sijui mtoto yule na mama yule wapo hai au la
maana hali zao zilikuwa mbaya sana kwakweli inauma sana''.
Alisema mhusika
aliyefanya tukio hilo ndiye anayejua alikuwa akimlenga nani lakini
hali hii inatisha na akawaomba wakristu wazidi kusali kwani inasikitisha
kuona matukio haya yanaendelea.
Alisema wakati
tukio hilo, linatokea kulikuwa na kulikuwa na ulinzi wa kutosha wa
polisi na awali walifanya na Balozi huyo wa Vatican hadi Ngorongoro .
“ kwatukio hili linatuhuzunisha sana tena kutokea mbele ya mgeni wetu”alisema Lebulu.
Askofu Malasusa atoa tamko
Askofu Mkuu wa
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa,
ambaye aliambatana na Makamu wa Rais ,Dk Ghalib Bilal wakitokea mkoani
Shinyanga, alisema amesikitishwa sana na tukio hilo.
Alisema tukio
hilo sio la kawaida na limewashtua watu wengi wanaopenda amani lakini
amewaomba waendelee kuwa watulivu wakati suala hili linapoendelea
kufanyiwa uchunguzi.
"Wakristo tuendelee kuhubiri amani, kuombea amani kwa sababu Mungu wetu ni wa amani,"
Makamu wa Rais atoa pole
Naye
Makamu wa Rais,Dk Bilal akizungumza baada ya maelezo hayo alitoa pole
kwa maaskofu hao na watanzania kwa ujumla kutokana na tukio hilo.
Hata hivyo,
aliahidi kuwa Serikali itajitahidi kuhakikisha wote waliohusika na tukio
hilo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola.
“serikali inatoa pole kwa tukio hili bay asana lakini tunaahidi
tutahakikisha waliohusika kupanga shambulio hili na kutekeleza
wanakamatwa”alisema Bilal.
Naibu waziri Nyarandu atoa misaada ya madawa ya milioni 16 na vyandarua
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu jana alitembelea
hospitalini ya Mount Meru na kuwapa pole majeruhi waliopa madhara
mbalimbali akiongozana na viongozi mbalimbali wa Mamlaka ya Hifadhi za
Taifa Tanzania (TANAPA).
Nyalandu
alikabidhi msaada wa Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) kwa waathirika
wa tukio hilo wa mablangeti 50 yenye thamani ya Sh 2.3 milioni na
fedha taslimu kiasi cha Sh 16.2 milioni kwaajili ya kununulia dawa
pamoja na vifaa mbalimbali vyakuhudumia wagonjwa hao.
''Nimefika hapa
nimehuzunika kwani nimekuta watoto wameumia sana nawapa pole wote
waliofikwa na tukio hili na zaidi nawaombea wapone lakini pia
nawapongeza madaktari na wauguzi kwa huduma wanazozitoa pia nawaomba na
wengine wajitolee kutoa misaada mbalimbali ili kuokoa maisha ya watu
hawa'',
Alisema
Inasikitisha kuona watoto wakiwa wameumia pamoja na watu mbalimbali
lakini zaidi ni mtoto wa miaka mitatu Kelvin Njau ambaye ameumia sehemu
za miguu huku mama yake akishindwa kuelezea tukio hilo na kuanza kulia.
Naye Dk ,Mariam
Murtaza ambaye ni Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru
aliishukuru wizara kwa msaada huo pamoja na wadau mbalimbali
wanaojitokeza kuchangia damu pamoja na vifaa mbalimbali ili kuokoa
maisha ya wahanga hao .
Dk Murtaza Pia
aliwapongeza madaktari,wauguzi na wataalam mbalimbali kwa ushirikiano
wanaoendelea kuuota na kuwaomba waendelee kuwa na ushirikiano kama huo
pale yanapotokea majanga mbalimbali.
No comments:
Post a Comment