Meneja Mauzo wa Airtel mikoa ya Tanga na Kilimanjaro Bw. Edmund Lasway akikabidhi baadhi ya vitabu vya sekondari kwa afisa elimu wa wilaya ya korogwe Bw. Shaaban Shemzighwa ikiwa ni msaada ulitolewa kuchangia elimu toka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa shule 4 za sekondari mkoani Tanga ikiwemo Korogwe Girls, Mkuzi Juu, Kwendimu na Magila, anaeshuhudia wakwanza kulia ni Bi Anesia Mauka- Mkuu wa shule Korogwe Girls. Hafla ya makabidhiano ilifanyika mwishoni mwa wiki katika shule ya sekondari Korogwe Girls mkoni Tanga
Kulia ni Afisa elimu wa wilaya ya korogwe Bw. Shaaban Shemzighwa ikimkabidhi kati ya vitabu vilivyotolewa kwa lengo la kuchangia elimu toka kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa Bi Anesia Mauka- Mkuu wa shule Korogwe Girls. Mwishoni mwa wiki Airtel ilitoa vitabu kwa shule 4 za sekondari mkoani Tanga ikiwemo Korogwe Girls, Mkuzi Juu, Kwendimu na Magila,. Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika shule ya sekondari Korogwe Girls mkoni Tanga.
*********
Kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel Tanzania imetoa msaada wa itabu vya hesabu,chemistry na baologia vyenye
thamani ya shilingi milioni 12 kwa shule nne za mkoa wa Tanga.
Msaada huo ni sehemu ya mpango wa
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel wa kusaidia ukuaji wa sekta ya limu
kupitia kampeni yake ya shule
yetu.
Akipokea vitabu hvyo
kwa niaba ya shule za mkoa wa tanga afisa elimu
wa wilaya ya korogwe
Bw. Shaaban Shemzighwa alisema,“ tunawashukuru Airtel kwa msaada huu wa vitabu
kwani utasaidia kupunguza tatizo lauhaba wa vitabu kwa shule zilizopatiwa
msaada huo na kuongeza kiasi cha ufaulu kwa wanafunzi. Tunaomba juhudi hizi
zisihishie hapaziendelea katika shule mbalimbali mkoani hapa na mikoa mingine
yaTanzania ili kuondoa ujinga na umaskini na kuwapa watoto wetu elimu bora
kwani hawa ndio taifa la kesho.
Kwa upande wake
meneja mauzo wa Airtel mikoa ya Tanga na Kilimanjaro Bw. Edmund Lasway amesema msaada
huo ni sehemu ya mpango wa kampuni yake
wa kusaidia ukuaji wa elimu hapa nchini. Chini ya mpango maalumu wa Shule yetu
tumeweza kuzifikia shule nyingi za sekondari nchini.
Akiongea kwa niaba
za shule zilizopokea msaada huo Mwalimu mkuu wa shule ya secondari
ya Mkuzi juu Bwn Victor Mwenda alisema” Tunatoa shukurani kwa Airtel
kwa msaada wa vitabu katika shule zetu zasekondari, kwa hatua hii itasaidia
kupunguza tatizo la vitabu linalozikabili na kuongeza ufanisi katika masomo ya
sayansi. Tunawaomba wanafunzi wavitunze na kuvitumia vizuri hivi vitabu kwani
ni nyenzo muhimu
katika elimu ya sekondari.
Vilevile Meneja wa
huduma za jamii wa Airtel Tanzania Bi Hawa Bayuni alidokeza kuwa
Airtel iko katika mkakati wa kuanza awamu nyingine ya ugawaji wa vitabu
kwa shule za sekondari kwenye kila mkoa ikiwa ni program yake ya mwaka huu ya
kurudisha kwa jamii kupitia elimu “tunaingia katika awamu ya mpya ya utowaji wa
vitabu kwa shule ngingi zaidi kila
mkoa hapa Tanzania, mradi wetu huu utazingatia zaidi shule za sekondari
zilizopendekezwa na Wizara ya Elimu kwamba ni shule zipi zina uhitaji
mkubwa wa vitabu na kushauri ziingie katika mpango wa kusaidia jamii wa
Airtel shule yetu” alieleza Bayumi.
Airtel toka
tulivyooanza mradi huu wa Vitabu miaka nane iliyopita tumeweza kuzifikia zaidi
ya shule 1500 za sekondari zilizopo Tanzania kwa kutoa msaada sawa kwa mikoa
yote na kuwafikia wanafunzi katika kila kona ya
Tanzania na pia kukarabati miundombinu ya shule kwenye maeneo mbalimbali
hapa nchini ikiwa ni hatua ya Airtel kukuza kiwango cha elimu kwenye
maeneo mbalimbali Tanzania aliongeza Bayumi.
Shule zilizofaidika
na msaada wa vitabu hivi mkoa ni Tanga ni pamoja na shule ya sekondari ya
Korogwe Girls, Mkuzi Juu, Kwendimu na Magila.mkakati ni kuendelea kutoa vitabu
kwa shule mbalimbali nchini ambapo droo ya shule za sekondari zitakazo faidika
na vitabu kwa mwaka huu wa 2013 -2014 itafanyika mwenzi Juni na kutoa
nafasi kwa shule nyingine nyingi za sekondari nazo kufaidika na mpango huu wa
Airtel shule yetu.
No comments:
Post a Comment