May 02, 2013

TWIGA BANCORP WALIVYOIFURAHIA SIKU KUU YA WAFANYAKAZI DUNAINI MEI MOSI 2013

 Mei Mosi ya kila mwaka hutumiwa na Wafanyakazi Duniani kote katika kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duaniani na Tanzania ni moja ya nchi ambazo zinaungana na Wafanyakazi Duniani Kote katika kuadhimisha siku hiyo. Twiga Bancorp ambayo ni taasisi ya fedha inayomilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 nayo ilishiriki katika maadhimisho hayo chini ya Mwanvuli wa TUICO. 

Wafanyakazi wa Twiga Bancxorp kupitia Chama cha wafankazi sehemu ya Kazi (TUICO tawiu la Twiga Bancorp walishiriki kikamilifu katika maadhimisho hayo. 

Mbali na kushiriki katika maandamano ya maadhimisho ya Kimkoa pia wafanyakazi hao walio kuwa wamejawa na furaha kutoka na na mazingira bora ya kazi walijumuika vyema na picha zifutazo zitakupa kile kilicho jiri.

 Wafanyakazi walifungua Shampeni kujipongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya kuwahudumia wananchi huku Mwajiri wao mkuu ambaye ni serikali ikiwajali.
 Wafanyakzi na viongozi wa Twiga Bancorp wakigonganisha glasi zao kuashiria umoja na Mshikamano wao walionao na pamoja na kutakiana heri na fanaka katika mwaka mpya wa kazi ulioanza jana.
 furaha ilikuwa ni kwa kila mfanyakazi wa Twiga Bancorp jijini Dar es Salaam
 Maandamano yakiendeleaaa
 Badru nae alionesha matunda ya Mfanyakazi ambaye anamazingira bora ya kufanya kazi ofisini ni pamoja na kuwa na wasaa na majukumu ya Kifamilia kama haya...
 Maandalizi ya Maandamano yakiandaliwa...
 Ni raha tu kwa wafanyakazi wa Twiga Bancorp hasa kutokana na mazingira mazuri na Bora ya kazi pamoja na kujivunia huduma bora kwa wateja wao.
 Wafanyakazi wa Twiga Bancorp kutoka matawi mbalimbali ya Benki hiyo Jijini Dar es Salaam wakipita mbele ya Mgeni Rasmi wakati wa maandamano ya Wafanyakazi katika Maadhimisho ya Meoi Mosi kimkoa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Furaha ndio kitu kilicho tawala katika matembezi hayo kama anavyo onesha mikogo dada huyu!!!
Baadhi ya wafanyakzzi wa Twiga Bancorp walioshiriki matembezi ya Siku ya Wafanyakazi iliyoadhimishwa kimkoa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana wakipiga picha ya poamoja.
Wafanyakazi wa Benki ya Twiga Bancorp wakiserebuka kwa muziki mara baada ya tafrija hiyo ya kupongezana na kuanza Mwaka mpya wa Kazi.

No comments:

Post a Comment