May 02, 2013

BARCLAYS TANZANIA YATOA SHS. 61 MILLIONI KWA BAYLOR TANZANIA KUSAIDIA VIJANA WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI (HIV/AIDS)

 002 Mkuu wa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Benki ya Barclays Tunu Kavishe,akikabidhi hundi ya Sh 61 Milioni kwa Mkurugenzi wa Mradi wa Chuo cha Utabibu  Baylor Dk Lumumba Mwita(kushoto)wakati wa makabidhiano yaliyofanyika  jijini Dar es Salaam jana,ambapo fedha hizo zitasaidia vijana wanaoishi na Virusi vya Ukimwi. 
 **********
 Benki ya Barclays Tanzania jijini- Dar Es Salaam imetangaza udhamini wa shillingi za kitanzania milioni 61 (TZS 61,000,000) kusaidia klabu ya Baylor Tanzania iliyoundwa kwa vijana wa umri wa kati wanaoiishi na virusi vya ukimwi na sehemu ya Chuo cha Utabibu cha Baylor cha Mfuko wa Watoto Tanzania (Baylor-Tanzania), asasi hiyo isiyo ya kiserikali, iliyosajiliwa chini ya muungano kati ya serikali ya Tanzania, USAID na Chuo cha Utabibu cha Baylor.

Baylor – Tanzania hufanya kazi Kanda ya Ziwa na Nyanda za juu Kusini, katika kituo cha kliniki ya watoto (Children’s Clinical Centers of Excellence (COEs)) kilichopo Mwanza (kilichojengwa kwa msaada wa Bristol Myers Squibb Fundation) na Mbeya (kilichojengwa kwa msaada wa mfuko wa Abbott). 

Baylor Tanzania ni sehemu ya mtandao ulioenea Afrika: asasi hii anzilishi ya kimataifa ya kushughuikia masuala ya ukimwi wa watoto  (Baylor International Pediatric AIDS Initiative (BIPAI)), huendesha vituo vya kliniki za watoto na kliniki nyinginezo katika nchi kumi na mbili za jangwa la Sahara Afrika na vile vile Romania, na inajishughulisha na kutoa huduma za kinga ya afya ya mtoto, kimsingi HIV, kifua kikuu, malaria, ukosefu wa lishe na sababu za kawaida zinazosababisha magonjwa ya watoto.

Watoto zaidi ya laki moja (100,000) na watu wazima wameshazipokea huduma za BIPAI tangu mwaka 1996, na kukifanya kuwa chuo kikuu kikubwa duniani kinachojihusisha na maendeleo ya afya ya mtoto.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo, Bi. Tunu Kavishe, Mkuu wa mawasiliano na Huduma za jamii  wa Barclays Tanzania amesema, “Benki ya Barclays hujali umuhimu wa uraia kwa umakini na kutambua hilo kama ufunguo wetu wa kibiashara. Tunapendezwa kufanya kazi pamoja na klabu ya vijana ya Baylor kuwapa nguvu vijana walioathirika na virusi vya ukimwi (HIV) na kuwa na uelewa chanya, kukuza mioyo yao na kuendeleza umuhimu wao kamili katika kupata ujuzi wa maisha, uzoefu mbalimbali, umuhimu wa utu uzima wa kuigwa na kazi maalumu, mwishowe kuwaongoza kukuza maendeleo yao ya kikliniki na kiakili katika muendelezo wa kuelekea utu uzima”.

Mkurugenzi wa mradi kutoka Chuo cha Utabibu cha Baylor ambae hufanya kazi pamoja na vijana wa klabu Dk. Lumumba Mwita alisema “kuwapa kinga madhubuti ya virusi vya ukimwi vijana wanaopevuka huhitaji msaada mkubwa wa kijamii kutoka katika familia, vijana wenye umri sawa na wao na watu wazima wa mfano - kuwashawishi tiba halisia, kuwa wawazi, lishe bora na tabia nyingine za kiafya. Vijana wanaoishi na virusi vya ukimwi (HIV) wana mahitaji yao mahususi lakini mahitaji hayo maranyingi hayafikiwi kwa sababu mbalimbali zikiwemo zile za kinga na mipango ya misaada ambayo mara nyingi hujengwa kwa watu wazima na kwa afya za watoto.

Klabu ya Baylor hutoa elimu ya jinsi gani ya kuishi na virusi vya ukimwi na huwaaminisha  walengwa kwamba kuna maisha ya kuishi dhidi ya virusi vya ukimwi. Pia huwa ni sehemu ya kupata uhakiki, umri kamili wa kuanza mapenzi na maelezo ya afya ya uzazi, ujuzi wa maisha ukiwemo uongozi na maendeleo, utoaji maamuzi, kupambanua ujuzi, mawasiliano, miradi inayozalisha kipato cha ziada na mengine mengi. Aliongezea “tungependa kutanguliza shukrani zetu za dhati kwa  Benki ya Barclays Tanzania kwa kutambua umuhimu wa kufanya kazi na Baylor na kutusaidia katika fedha za kuendelea kujiendesha na kuwapatia ujuzi sahihi vijana”.

Baylor Tanzania hivi sasa husaidia Klabu Wanachama za Vijana zaidi ya mia sita (600) Kanda ya Ziwa na Nyanda za juu Kusini – namba hii inatarajiwa kuongezeka kadri watoto wanaoishi na virusi vya ukimwi kutambuliwa, kuandikishwa katika tiba na kuishi katika umri huo na zaidi.

No comments:

Post a Comment