May 06, 2013

NYALANDU AWAJULIA HALI MAJERUHI WA MLIPUKO WA ARUSHA NA KUKABIDHI MADAWA YA MILIONI TSH 16

Naibu Waziri wa mali asili na Utalii Lazaro Nyalandu mtoto ambaye ni majeruhi aliyeathiriwa maeneo ya tumbo katika mlipuko wa bomu ,akimtembelea majeruhi walioathirika na shambulio la bomu bomu lililofanywa jana na mtu asiyejulikana katika ibada ya uzinduzi wa parokia mpya ya Mtakatifu Joseph iliyoko kata ya olasiti mkoani Arusha uliokuwa ukfanywa juzi na kusitishwa baada ya tukio hilo.Jumla ya watu 40 walijeruhiwa .Kulia ni Sister Beatrice Mndemo ambaye ni Muuguzi Msimamizi wa idara ya upasuaji.
****     *******
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu jana alitembelea hospitalini ya Mount Meru na  kuwapa pole majeruhi waliopa madhara mbalimbali akiongozana na viongozi mbalimbali wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).


Nyalandu alikabidhi msaada wa Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) kwa waathirika wa tukio hilo wa  mablangeti 50 yenye thamani ya Sh 2.3 milioni  na fedha taslimu kiasi cha Sh 16.2  milioni kwaajili ya kununulia dawa pamoja na vifaa mbalimbali vyakuhudumia wagonjwa hao.

''Nimefika hapa nimehuzunika kwani nimekuta watoto wameumia sana nawapa pole wote waliofikwa na tukio hili na zaidi nawaombea wapone lakini pia nawapongeza madaktari na wauguzi kwa huduma wanazozitoa pia nawaomba na wengine wajitolee kutoa misaada mbalimbali ili kuokoa maisha ya watu hawa'',

Alisema Inasikitisha kuona watoto wakiwa wameumia pamoja na watu mbalimbali lakini zaidi ni mtoto wa miaka mitatu Kelvin Njau ambaye ameumia sehemu za miguu huku mama yake akishindwa kuelezea tukio hilo na kuanza kulia.

Naye  Dk ,Mariam Murtaza ambaye ni Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru aliishukuru wizara kwa msaada huo pamoja na wadau mbalimbali wanaojitokeza kuchangia damu pamoja na vifaa mbalimbali ili kuokoa maisha ya wahanga hao .

Dk Murtaza Pia aliwapongeza madaktari,wauguzi na wataalam mbalimbali kwa ushirikiano wanaoendelea kuuota na kuwaomba waendelee kuwa na ushirikiano kama huo pale yanapotokea majanga mbalimbali.

Naibu Waziri wa mali asili na Utalii Lazaro Nyalandu mtoto ambaye ni majeruhi aliyeathiriwa maeneo ya tumbo katika mlipuko wa bomu ,akimtembelea majeruhi walioathirika na shambulio la bomu bomu lililofanywa jana na mtu asiyejulikana katika ibada ya uzinduzi wa parokia mpya ya Mtakatifu Joseph iliyoko kata ya olasiti mkoani Arusha uliokuwa ukfanywa juzi na kusitishwa baada ya tukio hilo.Jumla ya watu 40 walijeruhiwa .Kulia ni Sister Beatrice Mndemo ambaye ni Muuguzi Msimamizi wa idara ya upasuaji. Picha: Ferdinand Shayo.

No comments:

Post a Comment