May 05, 2013

MAKAMU WA RAIS TANZANIA, ASKOFU MKUU WA KKKT WAWAFARIJI MAJERUHI WA MLIPUKO ARUSHA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mtoto Kelvin Albert (3) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha. Kushoto ni Mama wa mtoto huyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mtoto Deric Siprian Kessy (8) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha. Kushoto kwa Makamu ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mwilongo na (kulia) kwa Makamu wa Ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Tanzania, Dkt. Alex Malasusa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mtoto Gabriel Godfrey (9) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali Restuta Alex (50) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimjulia hali mmoja kati ya wagonjwa waliokuwa mahututi, aliyelazwa katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji Askofu Mkuu wa kanisa Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti, Josephat Lebulu, wakati alipowasili nyumbani kwa askofu huyo jijini Arusha jana kumfariji kutokana na tukio la mripuko wa bomu lililotokea jana mchana, jijini Arusha kwenye hafla ya uzinduzi wa Kanisa hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi wa Vatcan na mwakilishi wa papa Francis, Askofu Francisco Montecillo, walipokutana nyumbani kwa Askofu Mkuu wa kanisa Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti, Josephat Lebulu, alipofika kumfariji kutokana na tukio la mripuko wa bomu lililotokea jana mchana, jijini Arusha.

1 comment:

  1. AnonymousMay 06, 2013

    Ninaungana na Watanzaniawenzangu kuwatakia faraja ya Mungu ndugu zetu waliofiwa na ndugu zao ktk mlipuko wa Arusha. Pia ninawaombea majeruhi Mungu awape uponyaji wa haraka.

    Ninaomba kwa ajili ya amni ya nchi yetu na pia Mungu atusaidie kuwapata haraka wahusika wa mlipuko na kujua nia na mipango yao juu ya kuhatarisha amni ya nchi yetu.

    MUNGU AIBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.

    Mchg. Fadhili J. Lyamuya

    ReplyDelete