May 05, 2013

MTU MMOJA AFA NA WENGINE 49 WAJERUHIWA KATIKA MLIPUKO WA BOMU KANISANI ARUSHA TANZANIA



MTU mmoja ambae hajafahamika jina lake ameuwawa , mtoto mmoja hali yake ni mbaya na yu  mahututi na wengine zaidi ya 49 wakiwa wamejeruhiwa vibaya katika tukio la kulipuka bomu majira ya saa  4,Asubuhi leo  wakati wa sherehe za ufunguzi  wa kanisa jipya la Mt joseph,la Roman Katoliki, lililopo Olasiti jijini Arusha.

Ufunguzi wa kaisa hilo ulifanywa na balozi wa Vatikan nchini, Fransisko  Padika,aliyekuwa ziarani mkoani Arusha, akiongozana na askofu wa jimbo kuu katoliki , Josephat  lebulu,  na kuhudhuriwa na waumimi wa makanisa ya Roman katoliki yaliyopo jijini Arusha.

Waumini waliojeruhiwa katika tukio hilo ambao wamelazwa katika hospital za  maunt Meru, na hospital teule ya jiji la Arusha ya St Elizabethi , wametambulika kuwa ni John Thadei,Regina   Fredirik, Joram  kisera, Novelt  John, Rose  pius, John  James,Anna Kessy, Joan Temba, Neema kihisu, Regina Fredirik, Joram Kisela, Vovalt  John, Gloria Tesha, Inocent Charles, Fatuma Haji, Fikiri Keya, John James, Anna Kessy, Simon Andrew, Anna Edward.
Wengine ni Lioba Osward , Ropse Pius, Philimon Gereza, Kisesa Mbaga, Neema Daud, Beata Cornel na Debora Joachim

Mkuu wa mkoa wa  Arusha, Magesa Mulongo ,  ameagiza vyombo vya ulinzi na  usalama mkoani humo kuhakikisha waliohusika kulipua bomu hilo wanatiwa mbaroni mara moja.

Wakati huo huo  jeshi la polisi limelazimika kutumia mabomu kumnusuru  mwendesha boda boda mmoja katika eneo hilo anayedaiwa alimtorosha mtu anayesadikiwa alirusha bomu hilo lililoaangukia mbele ya kanisa hilo na kujeruhi waumini hao.

Taarifa kutoka katika eneo la tukio zimesema kuwa wakati wa tukio hilo walifika watu wawili wakiwa na pikipiki, na kutoa kitu kilichorushwa wakati wa kukatwa utepe wa uzinduzi wa kanisa hilo.

No comments:

Post a Comment