TAKRIBAN saa moja mabasi na
magari mengine ya mizigo makubwa kwa madogo yaliyokuwa yakitumia barabara kuu
ya Mombo –Same yakitoka Arusha, Moshi kwenda Dar es Salaam na Mengine Mikoa ya
Pwani, Dar es Salaam na Morogoro kuelekea Arusha yalikwama katika eneo la Mombo
Mkoani Tanga kufuatia kunasa katika shimo kwa gari la Mizigo aina ya Fusso.
Juhudi za kulinasua gari hilo
zilifanywa baina ya madereva na wakandarasi wanaojenga barabara hiyo Kampuni ya
Strabag ya Ujerumani na kufanikiwa kuleta moja ya magreda yake na kulivuta gari
hilo.
Baada ya kulitoa gari hilo
mafundi wa kampuni hiyo walimwaga kifusi katika eneo hilo ambalo limeharibika
vibaya na mvua zinazoendelea kunyesha nchini kote.
Baadhi ya abiria wakiwa chini wakitafakari namna ambavyo wataweza kupita eneo hilo.
Maofisa wa Kampuni ya Strabag wakijadiliana jambo wajkati zoezi la kulinasua gari hilo likiendelea.
Abiria wakiwa hawana la kufanya..
Gari hilo aina ya Fusso likiwa limekwama..
Eneo ambali lilikwama gari hilo...
Nyororo ikifungwa tayari kulinasua gari hilo.
Hili nalo lilikwama na kusukumwa kidogo..
Abiria wakirejea katika mabasi yao kuendelea na safari...
No comments:
Post a Comment