Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipokea sehemu ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh. Milioni 35,
kwa ajili ya vijana wa Haraiki ya Mbio za Mwenge utakaowashwa Visiwani
Pemba Mei 6, mwaka huu, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za
Serikali wa Benki ya NMB, Domina Feruzi, wakati wa makabidhiano hayo
yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Mei
2, 2013. Kushoto ni Meneja wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa benki
hiyo, Elieza Msuya.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na wageni wake kutoka Benki ya NMB, baada ya makabidhiano
ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh. milioni 35 kwa ajili ya
vijana wa Haraiki wa mbio za Mwenge unaotarajia kuwashwa Mei 6, mwaka
huu Visiwani Pemba.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali
wa Benki ya NMB, Domina Feruzi (wa pili kulia) Meneja wa Kitengo cha
Huduma za Serikali wa benki hiyo, Elieza Msuya (kulia) Ofisa Mahusiano
wa benki hiyo, Doris Kilale (wa pili kushoto) na Huruma Mwaihomba, Ofisa
Mahusiano wa benki hiyo, baada ya makabidhiano hayo.
No comments:
Post a Comment