May 03, 2013

KUMBUKUMBU YA SARAH .L. GELLEGE


Leo mama yetu mpendwa imetimia miaka 2 kamili tangu uitwe na MUNGU.
Kwakweli ni ngumu kuzoea kuishi bila wewe lakini tunamshukuru sana sana MUNGU kwani anazidi kutupigania na kututia nguvu kwani ndio tegemeo letu. Pengo uliloliacha kamwe halitozibika kwani tunakumbuka ucheshi wako na juhudi zako na ushauri wako katika kupambana na maisha na tuliona juhudi zako mama!!

Unakumbukwa sana na wanao Luther(Mtua), Lamson(Ipyana) na Ruth. Pia unakumbukwa sana na wajukuu zako ambao hawaachi kuuliza bibi wa Ukonga mbona haji siku hizi kwani kaenda wapi? Unakumbukwa sana pia na dada zako,kaka zako,wadogo zako,wifi zako,shemeji zako,wajukuu zako,
watoto zako,wakwee zako,ndugu,jamaa,majirani na marafiki kwakweli wanakumiss sana!!!
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE!!!!.

No comments:

Post a Comment