April 29, 2013

WASANII BONGO FLEVA WAFUNIKA KAMPENI YA AIRTEL YATOSHA JIJINI MWANZA

 Ney wa Mitego, The True Boy himself.
 
WASANII wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Fleva)  wamefunika kwa kutoa burudani ya nguvu kwenye kampeni inayoendeshwa na Kampuni ya Airtel nchini ya airtel yatosha  na kuwapa raha maelfu ya wapenzi wa muziki huo waliofurika katika  viwanja vya wazi vya Furahisha Jijini Mwanza.

Kampeni hiyo ya siku mbili iliyofanyika katika viwanja hivyo na kushuhudia na maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Mwanza kupata ushuhuda wa Airtel yatosha kwa kununua laini za simu za mkononi za Kampuni hiyo na jinsi ya kutumia huduma ya Internet, kuongea kwa kujiunga na kupata dakika nyingi za muda wa maongezi kwenda mitandao mingine kwa bei nafuu zaidi kwa laini moja tu ya Airtel.

Wasanii wa Bongo Fleva waliotoa burudani na kuwaacha hoi maelfu ya wananchi waliofurika kupitia vibao vyao vinavyotamba kwenye vituo mbalimbali vya redio na televisheni hapa nchini ni pamoja na Juma Kassim ‘Nature’ na kundi lake la Wanaume Halisi, Roma Mkatoliki, Madee na Ney wa Mitego.

Maelfu ya wananchi walioshuhudia kampeni hiyo waliweza pia kushuhudia vipaji vya uimbaji kutoka kwa vijana walioshindanishwa na waliojitokeza kucheza muziki wa Bongo fleva katika viwanja hivyo na
kupata zawadi ya laini na fulana (T-shirt) za Kampuni ya Airtel zilizotolewa kwa washindi waliopatikana.

“Wananchi wengi wamekuja hapa kupata burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongo fleva kama ulivyojionea lakini pia wengi kwa sasa wanatumia mtandao wa Airtel ikiwemo huduma hii ya Airtel yatosha pamoja na kununua laini na kupatiwa maelezo ya jinsi ya kutumia huduma hii”alisema msanii Ney wa Mitego.

Akizungumzia Kampeni hiyo Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo Jackson Mmbando alisema kwamba tangu kuzinduliwa na kufanyika  katika mikoa sita hadi sasa hapa nchini kumekuwa na mapokeo na mafanikio makubwa kwa kuongeza wateja wanaotumia mtandao wa Airtel kupitia huduma zote.

Mfanyabiashara wa vituo vya kuuza mafuta Barnabas Mathayo wa Jijini Mwanza alitoa ushuhuda wa kukubali huduma inayotolewa na Airtel katika mahojiano maalumu alisema kwamba tangu kuanzishwa kampeni ya Airtel yatosha amekuwa akinunua kifurushi na kujiunga na kujipatia muda wa kutosha kufanya mawasiliano na ndugu, rafiki, wavuvi wanao nunua mafuta kwaajli ya boti zao pamoja na wafanyabiashara mbalimbali kupitia mitandao yote kwa bei ile ile.
 
“Huu ni Mkoa wa sita sasa na kama mlivyoshuhudia wingi wa watu wanaokuja kushuhudia burudani na kupata maelezo ya jinsi ya kutumia mtandao huu kwa garama nafuu zaidi na ikizingatiwa Mkoa wa Mwanza ni moja ya mikoa inayojishugulisha na uvuvi, kilimo, ufugaji na wafanyabiashara kutoka ndani na nchi za maziwa makuu”alisema Meneja huyo.

“Hatukaangi laini ni moja tu yatosha zingine za nini na ukiangalia Mwanza ni Mkoa wa burudani, biashara, viwanda, kilimo, uvuvi na ufugaji hivyo wananchi wake hawana budi kutumia mtandao wa Airtel ambao umedhamiria kuwainua kiuchumi na kuletwa kwa kampeni hii itawasaidia kujifunza Airtel kuna nini ndani ya mtandao huu”alisema

Mbando aliongeza kuwa kampeni hiyo inaendelea katika Mikoa ningine na mwishoni mwa juma hili kampeni hiyo itahamia Jiji kubwa la Dar es salaam katika viwanja vya Zakhem na kutakuwa na burudani ya kukata na  shoka kutoka kwa wasanii mbalimbali kutokana na wasanii wengi kuwa jijini humo na kutoa wito kwa wananchi kufika kushuhudia na kujifunza ndani ya mtandao wa Airtel kuna vitu gani na kwa gharama nafuu.
 Mashabiki wa True Boy, Ney hawakuwa nyuma
 Msanii Chipukizi aliyeonyesha kipaji cha hali ya juu kwa kughani mashairi yenye mvuto kwa miondoko ya HIPHOP wa mkoani Mwanza maarufu kwa jina la Dogo D alifanya burudani kali katika tamasha maalum la
Airtel yatosha mkoani Mwanza katika viwanja vya Furahisha
Ujumbe kutoka kwa wananchi unasomeka
 Roma kazini
 Roma Mkatoliki, baada ya kuwatosheleza kwa burudani wakazi wa Mwanza
Madee kutoka Manzese...

No comments:

Post a Comment