Watangazaji wa kipindi cha Guinness Football Challenge Larry Asego(kulia) na Flavia Tumsiime(kushoto).
Washindi wa kipindi cha Tatu cha Guinness Football Challenge,Kenneth Kamau(kulia) na Wills Ogutu (kushoto) wote wanatoka Nairobi Kenya, katika picha ya pamoja na watangazaji wa kipindi hicho Larry Asego na Flavia Tumsiime.
******* ********
Katika sehemu ya tatu jana usiku kupitia
televisheni za ITV na Clouds TV, mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ yalionesha
ni jinsi gani utulivu unavyosaidia katika mashindano ambapo timu kutoka Kenya
ilifanikiwa kuzitoa timu nyingine za Tanzania, Uganda na timu nyingine kutoka
Kenya .
Kenneth Kamau na Wills Ogutu walishinda katika mikwaju ya penati na
kufikia hatua ya mwisho katika ukuta wa pesa wa Guinness ambapo walifanikiwa kulenga
matundu manne na kupata fedha za kimarekani dola 5,500. Kwa bahati mbaya
walishindwa kulenga tundu la mwisho na hivyo kupelekea kupoteza dola 2,500 na
kuondoka na fedha za kimarekani taslimu dola 3,000.
Kenneth
na
Wills wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya
Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia kitita cha fedha
za kimarekani hadi kufikia dola 250,000. Katika kipindi kijacho cha
mashindano haya kinachorushwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds
TV,
timu nne mpya zitaingia uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani
ataibuka
mshindi na kutambulika kama wachezaji na
si tu mashabiki,watatakiwa kushinda na kuziwakilisha nchi zao katika
mashindano
ya Pan-African.
GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya
Endemol. Kipindi hiki kinarushwa kila
Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV. Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia
saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku
ambapo Clouds TV itarusha kipindi
hicho saa mbili na dakika kumi na
tano(2:15) usiku .
Tafadhali kunywa
kistaarabu - Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.
No comments:
Post a Comment