April 04, 2013

MAREHEMU FATMA MDOE KUZIKWA MAKABURI YA KISUTU JIONI YA LEO

MDAU Said Mdoe amefiwa na  dada yao kipenzi Fatma Mdoe  (pichani) aliyefariki  ghafla jana (Jumatano) saa 10 jioni, msiba uko nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach, jirani na Dr Hizza.

Mazishi ni leo Alhamisi saa 10 Alasiri katika makaburi ya Kisutu, DSM. Msafara wa kutoka Mbezi kuelekea makaburini utaanza saa 8.30 mchana ili kukabiliana na adha ya foleni.

Mungu amlaze mahali pema peponi-Amen. 

No comments:

Post a Comment