DAR ES SALAAM, Tanzania
SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), linatarajia kushirkiki maonesho ya siku tatu ya Huduma za Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (The Muhimbili Day Exhibitions 2013), ambayo yanafunguliwa rasmi kesho Jumatano na Waziri wa Afya, Dk Hussein Mwinyi.
Maonesho hayo yanayoratibiwa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), yatafikia tamati Ijumaa Aprili 19, yakiwa na nia ya kutoa nafasi ya kukuza huduma zake kwa wateja wake, kwa kushirikisha taasisi na kampuni mbalimbali zenye udau katika sekta ya afya nchini.
Akizungumza na Habari Mseto, Ofisa Uhusiano wa NSSF, Maife Kapinga, alisema walipokea mwaliko wa ushiriki wa maonesho hayo kutoka MNH na kisha kuthibitisha, wakimiani ni fursa pana itakayotangaza huduma za shirika hilo ambazo zina uhusiano wa karibu na sekta ya afya.
Aliongeza kuwa, wanachama na wasio wanachama wa NSSF watapata fursa adhimu ya kujionea utoaji na uendeshaji wa huduma mbalimbali, zilizo na udau na Sekta ya Afya, kama vile Mafao ya muda mrefu na Mafao ya muda mfupi.
Aliongeza kwa kuyataja mafao ya muda mfupi kuwa ni pamoja kuumia kazini, ambapo kuna namna mbili za kuumia akizitaja kuwa ni kuumia kwa taratibu kunakotokana na kazi husika na kuumia kwa ghafla kama vile kukatika mkono na viungo vingine vya mwili.
Mafao ya Uzazi kwa akina mama, mafao ya rambirambi katika mazishi ya mwanachama, mafao ya uzeeni, mafao ya ulemavu haasa ulemavu utakaomtoa mwanachama moja kwa moja kazini, pamoja na ya mirathi, ambapo mke/mume na watoto ndiyo wanawajibika kumrithi mwanachama.
Maonesho hayo ya kila mwaka yanahusisha wadau wa afya wanaotoa huduma za matibabu na upasuaji, wataalamu wa mionzi, wafamasia, wamiliki wa maabara, maduka ya dawa, wasimamizi wa taarifa za kitabibu na huduma nyinginezo za kitiba.
‘Muhimbili Day Exhibitions’ ni maonyesho yanayotoa fursa ya kipekee kwa washiriki kuonyesha bidhaa na huduma zao, ambayo pia ni jukwaa kamili la kujenga mahusiabno ya kibiashara kati ya watoa huduma na wateja wao, ikiwamo kupokea maoni kutoka kwa watumiaji wa bidhaa zao.
No comments:
Post a Comment