April 17, 2013

NAPE AKATISHA ZIARA ASHIRIKI MAZISHI ULANGA


Katibu wa NEC-CCM Itikadi, Siasa na Uenezi, Nape Nnauye akiweka shada la maua kwa miaba ya chama hicho, wakati yeye na viongozi wengine walishiriki kwenye mazishi ya msiba wa marehemu Galus Matanji yaliyofanyika katika makaburi ya Kanisa la Katoliki Kalengakelo la Mtakatifu Petro, Kata ya Mtimbila, wilayani Ulanga, Morogoro jana. Nape ambaye alikuwa kwenye ziara ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama hicho, aliamua kusitisha baadhi ya shughuli na kuamua kushiriki misiba miwili iliyotokea eneo hilo ukiwemo wa Mwanaiba Seif. (PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

 Nape akimkabidhi ubani baba mzazi wa marehemu Mwanaiba Seif, Abdul Seif
Katibu wa NEC-CCM Itikadi, Siasa na Uenezi, Nape Nnauye, akishiriki katika maziko ya Mwanaiba Seif yaliyofanyika eneo la Kalengakelo, Mtibila wilayani Ulanga, Nape ambaye alikuwa kwenye ziara ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama hicho, aliamua kusitisha baadhi ya shughuli na kuamua kushiriki misiba miwili iliyotokea eneo hilo ukiwemo wa marehemu Galus Matanji.
 Katibu wa NEC-CCM Itikadi, Siasa na Uenezi, Nape Nnauye, na Mbunge wa Jimbo la Ulanga Magharibi, Dk. Hadji Mponda (CCM), wakiwa katika ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Matanji katika Knisa la Mtakatifu Petro.
Nape katikati akiwaongoza baadhi ya viongozi kwenda kushiriki ibada ya kuuombe mwili wa marehemu Matanji katika Kanisa la Katoliki
 Mbunge wa Ulanga Magharibi, Dk. Hadji Mponda (katikati)akitoa salamu za rambirambi katika maziko ya marehemu Matanji.
 Pape akishiriki katika maziko ya marehemu Matanje
                                    Nape akimkabidhi ubani mmoja wa wanafamilia ya marehemu Matanji.
 Marehemu Mwanaiba akizikwa

No comments:

Post a Comment