April 17, 2013

MAKAMU WA RAIS DK. BILALI AFUNGUA RASMI MKUTANO WA PAMOJA WA KIMATAIFA WA WATAFITI WANASAYASI AFRIKA JIJINI ARUSHA


Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali akifungua rasmi Mkutano wa Pamoja wa Kimataifa wa Watafiti Wanasayasi Afrika ulioandalia na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwa kushirikiana na Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Kuambukiza Kusini mwa Afrika (SACIDS) ya Afrika Kusini. Kushotoni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk. Mwele Malecela. Mkutano huo wa siku nne unafanyika Jijini Arusha.

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akiwa katika picha ya Pamoja na Washindi wa Tuzo za mwaka 2012 za Masuala ya Afya, Prof. Ester Mwaikambo (kushoto) na  Dk Martha Lemnge mara baada ya kuwakabidhi tuzo zao hii leo.

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal akiwa katika picha ya Pamoja na Washindi wa Tuzo za mwaka 2012 za Masuala ya Afya, Prof. Ester Mwaikambo (kushoto) na  Dk Martha Lemnge mara baada ya kuwakabidhi tuzo zao hii leo. Kulia ni Mkurugenzi wa NIMR, Dk. Mwele Malecela.
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu TanzaniaNIMR), Dk. Mwele Malecela akisoma hotuba yake.
 Badhi ya Watafiti Wanasayansi kutoka Taasisi zaidi ya 35 barani Afrika wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa NIMR wakati wa hotuba yake ya ukaribisho.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Kuambukiza Kusini mwa Afrika (SACIDS), Mark Rweyemamu akisoma risala yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo Jijini Arusha.
Viongozi wa NIMR na Watafiti mbalimbali wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa SACIDS.
 Mkurugenzi wa OHCEA, Japhet Kilewo akitoa hotuba yake.
 Meza kuu ikifuatilia kwa ukaribu Hotuba ya Mkurugenzi wa OHCEA.
 Mwakilishi kutoka Umoja wa Afrika (AU)Dk. Ahmed Hamdy akizungumza na Wanasayansi watafiti.
  Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid nae alisoma Hotuba ya Wizara na kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mkutano huo.
 Wakuu wa Taasisi za kitaifa na Kimataifa pamoja na wanasayansi watafiti wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.
 Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal pamoja na Mkurugenzi wa NIMR, Dk. Mwele Malecela wakizindua rasmi awamu ya nne ya Vipaumbele vya Tafiti za Afya kwa mwaka 2013-2018.
 Pia Makamu wa Rais alipata fursa ya kuzindua Mpango wa Afya Moja nchini Tanzania
Aidha Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal pia alizindua Mpango wa Uchunguzi wa Magonjwa ya Kuambukiza Kusini mwa Afrika (SACIDS).

No comments:

Post a Comment