Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto akimwelekeza bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' jinsi ya kupiga maumbwi ku kupangua ngumi za mpinzani wake |
BONDIA Ibrahim Class 'King Class Mawe' amendelea kujifua na kujiandaa kumkabili Amosi Mwamakula katika pambano la utangulizi wakati wa mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali.
Pambono la raundi nane linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi Siku ya jumatano , linatarajiwa kuwa la vuta nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema.
Kocha wa King Class Mawe, Rajabu Mhamila 'Super D' alisema kuwa bondia wake anajiandaa vema na
matumaini yanaonekana baada ya kucheza Sparng na watu watano tofauti
tofauto ambapo alianza kupambana na Abuu Mtambwe raundi 4,Kassimu
Gamboo, nae vile vile na Ibrahimu Toll pamoja na Ally Masaga kitu
ambacho kimenipa moli wa kumchakaza Mwamakula ili kuendelea kujiwekea rekodi nzuri.
"Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na Mashali" alisema Super D.
Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa katika mchezo huo kutakuwa na CD na DVD za mafunzo wa mchezo huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.
Aliongeza kuwa baadhi ya mapambano yaliyomo ni katika CD na DVD hizo ni ya Kalama Nyilawila dhidi ya Francis Cheka, Mbwana Matumla naFrancis Miyeyusho, Said Mundi na King Class Mawe. na Francis
Cheka dhidi ya Japhet Kaseba mapambano yote mawili mbali na hivyo
atakuwa akisambaza vifaa vya mchezo wa masumbwi kwa mabondia ambao awana
wanaweza kumuona na kujipatia vifaa mbalimbali
No comments:
Post a Comment