April 24, 2013

ENEO LA NYAMA CHOMA LUGONO SASA LINAHUDUMA SAFI YA KUCHIMBA DAWA

Muuzaji wa Mishikaki ya Nyama za kuchoma ya Mbuzi  katika eneo la biashara  Lugono linalotumiwa na  vijana wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Kata na Tarafa ya Mlali, Wilayani Mvomero  kwa uuzaji wa nyama choma, matunda, na bidhaa nyingine kwa wasafiri wanaotumia barabara kuu ya Morogoro, Iringa, Mbeya na Zambia akiwa tayari na mishikaki hiyo kwaajili ya kuwauzia wasafiri. Mshikaki mmoja huuzwa kwa shilingi 3,000/=.

Enbeo hilo ambalo zamani lilikuwa halkina huduma ya vyoo hivi sasa huduma hiyo inapatikana katika hali ya usafi kwa sh 200/= ambapo abiria na wasafiri wengine hutumia kwa kulipia.

Abiria wanaosimama eneo hilo wameombwa kutumia huduma hiyo ya vyoo na kuacha tabia ya kujisaidia vichakani. 



Abiria mbalimbali wakijipatia nyama choma safi ya mbuzi na ndizi za kukaanga. katika eneo hilo la Lugono.
Moja ya mabasi yafanyayo safari zake katika barabara ya Morogoro na Zambia likisubiri abiria wake.

Moja ya Majengo safi ya Vyoo yaliyopo katika eneo hilo.
Abiria wakielekea katika vyoo hivyo kujiweka sawa. 
 
Ingawa eneo hilo lina vyoo safi lakini bado abiria wasio wastaarabu kama hawa hapa huamua kuingia porini kujisaidia kwa kukwepa kulipa Tsh 200/=. Mmoja wa viongozi wa eneo hilo, Ngalai Mrefu ameiambia Blogu hii abiria wa namna hii wanawasumbua sana na wapo mbioni kuanzisha utaratibu wa faini kwa abiria yeyote atakae jisaidia porini.
Maj na soda pia vinapatikana katika eneo hili.

No comments:

Post a Comment