Mkurugenzi wa
Kamati ya Miss Tanzania kutoka kampuni ya Lino International Agency, Hashim
Lundenga na Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, Oscar Makoye (kushoto)
wakizungumza na Warembo wanaoshiriki shindano la kumtafuta Redd's Miss Dar
Indian Ocean linalotaraji kufanyika kesho jijini Dar es Salaam.
****** ******
Na Mwandishi Wetu
HATUA
za awali za kumsaka Redd’s Miss Tanzania sasa zinaanza kushika kasi,
wakati wiki hii kutakapokuwa na kinyang’anyiro katika vitongoji kadhaa
vya kusaka warembo wao.
Kazi
kubwa itaanza Morogoro, wakati atakaposakwa Redd’s Miss High Learning
atakayeuwakilisha mkoa huo katika kumpata mrembo kutoka Vyuo vya Elimu
ya Juu, shindano litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Sirvoy.
Wakati
Morogoro Miss High Learning akipatikana kesho, shughuli pevu ipo
keshokutwa (Jumamosi) pale kutakapokuwa na shindano la kumsaka Redd’s
Miss UDOM, litakalofanyika katika Ukumbi wa Kilimani, Dodoma.
Siku
hiyo pia atapatikana mwakilishi wa vyuo vya elimu ya juu kutoka Kagera
na Mwanza, shindano ambalo litafanyika Yacht Club, Mwanza.
Akizungumzia
kuhusu Redd’s Miss Morogoro High Learning, mratibu wa shindano hilo,
Verdian Kamugisha alisema kila kitu kimekamilika na kutakuwa na burudani
za kufa mtu.
“Tumekamilisha
kila kitu na warembo wote wako katika hali nzuri na kutakuwa na
burudani za kumwaga, wakazi wa Morogo wanatakiwa kuja kwa wingi
kushuhudia kile kitakachotukia,” alisema.
Mratibu
wa Shindano la Redd’s Miss UDOM, Rachel Matina naye alisema kila kitu
kwao kipo tayari na watu wanatakiwa kufika kwa wingi kushuhudia jinsi
warembo kutoka Chuo Kikuu Dodoma, walivyopania kulitwaa taji la Redd’s
Miss Tanzania mwaka huu.
Joseph
Rwebangira wa anayeratibu shindano la wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya
Juu kwa mikoa ya Kagera na Mwanza naye alikiri kukamilika kwa maandalizi
yote na kutakuwa na burudani za kila aina siku ya onyesho.
Upande
wa kanda ya kaskazini mwa nchi kutakuwa na shindano la kumsaka mrembo
wa kitongoji cha Hai ambapo shindano hilo linatarajiwa kufanyikia katika
ukumbi wa Hotel ya Snow View na mkoani Mara katika kitongoji cha Tarime
shindano litakuwa katika ukumbi wa JJ Club na maandalizi kwa sehemu
zote husika yameshakamilika kwa kiwango kikubwa.
Redd’s Miss Tanzania kwa sasa inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.
No comments:
Post a Comment