Gari dogo aina ya Toyota Rav4 L namba za Usajili T 363AKN likiwa limeparamia nyumba na kuvunja sehemu ya
fremu ya duka katika Nyumba ya Mama Lili iliyopo Ukonga Mazizini jinni Dar es
Salaam juzi. Ajali hiyo iliyotokea usiku wa manane haikuleta maafa zaidi ya
uharibifu wa mali.
Kwamujibu wa mashuhuda
wanasema kuwa gari hiyo iliyokuwa na watu wawili ndani yake na kuendeshwa na
mwanamke iliparamia nyumba hiyo baada ya kumshinda dereva huyo kutokana na
mwendo kasi.
Ilidaiwa gari hilo kutokea
maeneo ya Mombasa likiwa katika spidi kali na mara baada ya kumaliza barabara
ya lami lilimshinda dereva kutokana na mashimo na kupara mia nyumba hiyo baada
ya kuvuka mtaro.
No comments:
Post a Comment