Mkurugenzi Mtendaji
wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina, akizungumza na waanbdishi wa
habari Makoa Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam juu ya mchakato wa
Matembezio ya Hisani ya Step Ahead mwaka huu ambayo yatafanyika Juni 8, 2013 na
yatakuwa ya Kilometa 5 ambapo Mgeni Rasmni anataraji kuwa Dk. Asha-Rose Migiro.
Pamoja nae ni Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Susan Boon.
Mkurugenzi wa AMREF
Tanzania Dr, Festus Ilako (kulia) akizungumzia ushiriki wa Shirika hilo katika
kufanikisha matembezi hayo ya Hisani ya
Step Ahead mwaka huu ambayo yatafanyika Juni 8, 2013 na yatakuwa ya Kilometa 5
ambapo Mgeni Rasmni anataraji kuwa Dk. Asha-Rose Migiro. Pamoja nae ni Naibu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Susan Boon (kushoto) na Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Benki ya Barclays Tanzania, Tunu
Kavishe akifdafanua jambo kwa wanahabari juu ya matembezi hayo ya Hisani.
Wengine katika picha ni Naibu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT,
Susan Boon (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara
Maina.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari nchini Tanzania na Afrika Mashariki wakisikiliza kwa makaini uzinduzi wa matembezi hayo ya hisani ambapo nawao wamehimizwa kushiriki ili kuchangia Matibabu na afya ya mama na mtoto nchini.
**** ****
Kila mwaka Benki ya
Barclays inaandaa matembezi ya kuchangisha fedha yaliyobatizwa kwa jina la Step
Ahead Walk. Mchakato huu umekuwa ukiendelea toka mwaka 2006 na Tanzania
walifanya Step Ahead yao ya kwanza mwaka 2008 ambapo fedha zilichangishwa na zilitumika kusaidia
matibabu ya kansa kwa watoto kwenye kituo cha kansa cha Ocean Road.
Matembezi haya ya
hisani yajulikanayo kama Step ahead ni mkakati endelevu wa benki
ya Barclays ambapo kusudi lake ni kujenga uelewa wa kusaidia mahitaji
muhimu katika jamii. Tangu
ilipozinduliwa mwaka 2006, mkakati huu mhuu umeweza kusaidia kuelimisha
uchangishaji fedha ili kusaidia masuala ya uzazi na afya ya watoto wachanga–
ambayo ni muhimu kwa jamii yetu.
Akiongea katika
vyombo vya habari leo, Ndugu, Kihara Maina, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya
Barclays Tanzania amesema, tukio hili rasmi itafanyika tarehe 8 juni, 2013
katika hoteli ya Golden Tulip na litahusisha matemebzi ya hisani ya kilomita
tano (5) na kila mtu katika jamii anakaribishwa kushiriki. Tiketi zitauzwa kwa
shilingi za kitanzania 5000 na zitapatika katika kila tawi la Benki ya Barclays
kuanzia tarehe 29 Aprili, 2013
Susan Boon, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa CCBRT amesema “msaada huu ambao CCBRT wanaupokea kutoka Benki ya Barclays ni
wa thamani sana ambapo tunafanya kazi
ili kufikia malengo ya Tanzania ambapo jamii itajiwezesha kupaha huduma bora na
salama hasa kwa walemavu wa viungo na pia itawafikia wakinamama wote na
kuhakikishia usalama wao kwenye huduma
ya afya ya uzazi na watoto wachanga
inafanikiwa. Mkakati huu wa benki ya Barclays Step Ahead utasaidia pia katika
kukinga mapungufu ya mtindio wa ubongo na fistula hapa Tanzania, na vile vile kuhakikisha
kwamba wale waliopata mapungufu wakati wa kuzaliwa wanapata matibabu katika sehemu za viungo vyao haraka
iwezekanavyo.
Pia kwa kushirikiana
na taasisi zetu za hapa nchini CCBRT na benki ya Barclays Tanzania tunakusudia
kuwa mfano mzuri na muhimu katika jamii inayotuzunguka na tunafutrahia sana
kuwa chachu ya msaada katika jamii yetu inayotuzunguka ya Tanzania.”
Akiongea pia na
waandishi wa habari katika mkutano na vyombo vya habari, Dr, Festus Ilako
Mkurugenzi wa AMREF Tanzania amesema “Msaada na mkakati huu wa benki ya
Barclays Tanzania kwa AMREF ni wa kila wakati, na kwa pamoja tunaweza tukaibadilisha
jamii kutoka ilipo katika masuala ya afya kwa wakina mama na watoto, hivyo
kuitengenezea jamii uelewa na ustadi katika kusimamia afya njema na kuvunja
marudio rudio ya ufukara katika afya na
umaskini.
Kampeni hii kutoka
benki ya Barclays ijulikanayo kama Step Ahead itasaidia kuelimisha wakunga na
wazalishaji katika wilaya ya Kilindi mkoani Tanga na kuwawezesha wakina mama
wajawazito kujifungua katika mikono ya salama ya wafanyakazi waliofuzu katika
Nyanja ya afya hivyo kupunguza uchangiaji wa vifo visivyo lazima na ulemavu wa
viungo kwa mama na watoto chini ya miaka mitano. Ushirika huu baina ya Barclays na AMREF ni
mfumo mpya ambayo utawezesha jamii
kupata ubora na unafuu katika masuala ya kiafya.
Mwaka 2011, Benki ya
Barclays na washiriki wake walifanikiwa kuchangisha shilingi za kitanzania
milioni 150 kutokana na mauzo ya tiketi
na matoleo mengine kutoka kwa wafadhili. Mwaka huu lengo ni kuchangisha zaidi
ya marambili ya shilingi milioni 150 kutoka kwenye matoleo ya washirika muhimu
na washiriki wengine katika jamii.
Fedha zitakazochangishwa mwaka huu zitakwenda kusaidia katika masuala ya uzazi na afya ya watoto kama ifuatavyo:-
1. Mafunzo kwa wakunga wa uzazi
2. Matibabu ya Fistula
3.Upasuaji kwa watoto waliozaliwa na ulemavu
unaosababishwa na uzazi
Step Ahead Walk 2013
itaweza kufanikiwa tu kama itawezeshwa na kila mshiriki na jamii nzima ya
kitanzania kwa ujumla. Kwa sababu hiyo basi tujiunge wote ili tuweze kufanya
badiliko katika masuala ya afya kwa ujumla hapa Tanzania hususani masuala ya
uzazi na afya ya watoto.
No comments:
Post a Comment