March 28, 2013

WHO YAKABIDHI MSAADA WA VIFAA VYA SH.BILIONI 2.4




Naibu Katibu  Mkuu wa  Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi. Regina   Kikuli  akionesha  ufunguo wa gari wa moja ya magari saba  yaliyotolewa leo (jana) ,ambapo  ni msaada  kutoka WHO na vifaa vingine vyenye thamani ya sh. bilioni 2.4  katika hafla iliyofanyika  jijini Dar es Salaam. katika hafla iliyofanyika  jijini Dar es Salaam. Katika msaada huo magari mengine 22 yatatolewa baade.
****     *****
NA FRANK JOHN – MAELEZO


SHIRIKA  la  Afya  Duniani ( WHO) limekabidhi msaada wa  vifaa mbalimbali wenye thamani sh. bilioni 2.4  kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili  kusadia katika kupunguza vifo vya watoto wachanga walio chini ya miaka mitano na kuiwezesha Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) katika utendaji wake.

Msaada huo umetolewa leo (jana) na Mwakilishi Mkazi wa WHO Dk. Rufaro Chatora , ambapo alimkabidhi Naibu Katibu  Mkuu wa wizara hiyo, Bi. Regina   Kikuli  katika hafla iliyofanyika  jijini Dar es Salaam.


 Akikabidhi  msaada huo, Dk.  Chatora  amesema shirika hilo linathamini juhudi za serikali katika kupunguza vifo vya watoto ndio maana linaipongeza kwa kutimiza malengo ya milinea ambapo watoto wote wamefaidika na malengo hayo.

Alivitaja   baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni majokofu 128,komputa nne magari saba  ya aina mbalimbali mashine za kutolea kopi,vifaa vya kufuatilia ubaridi ndani ya majokofu yatakayotumika kutunza dawa kwa ajili ya chanjo  za watoto walio chini ya miaka mitano, vifaa  vingine kwa ajili ya kusaidia  TFDA.

Akizungumzia kuhusu msaada huo, Bi  Kikuli  alibainisha kuwa  umekuja kwa wakati muafaka ambapo serikali imekuwa ikishirikiana vyema na washirika wa maendeleo katika kutimiza malengo ya milenia hasa lengo la nne na tano  ambayo yanalenga kuboresha sekta ya Afya kwa kupunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano  kwa kuwapatia chanjo stahiki kwa wakati kwa kuwa   chanjo ni haki ya kila mtoto.

 Aliongeza kuwa serikali ya Tanzainia imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza malengo  ya milenia hasa lengo namba nne  ambalo ni kupunguza vifo vya watoto walio chini  ya miaka mitano, ambapo vifo hivyo vimepungua kutoka kutoka 147 kwa vizazi hai 1000 hadi 81 mwaka 1999  na vifo vya watoto chini ya mwaka mmoja kutoka 99 kwa vizazi hai 1000 hadi 51  katika  kipindi  cha mwaka 2010.

Bi .Kikuli alitumia nafasi hiyo kwa niaba ya serikali kuwashukuru wadau wa maendeleo na chanjo na kuwahakikishikia kuwa msaada huo utatumika kwa makusudio yaliyopangwa ili kusaidia kuboresha  afya za Watanzania hususan watoto.

No comments:

Post a Comment