Taarifa za awali kutoka Chama cha Wananchi CUF, zinasema kuwa Mwili wa Marehemu,
Khamis utaagwa kesho asubuhi kuanzia majira ya saa 2:30-4:00 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es
Salaam ambapo Viongozi mbalimbali wa kitaifa na Kimataifa pamoja na wananchi na
Wanachama wa CUF watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu.
Taarifa hiyo ya Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julis Mtatiro inasema kuwa
Msafara utaondoka Karimjee saa 4:00 kuelekea uwaja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere ambapo Msafara wa Ndege 2 utaondoka kwenda Pemba.
Saa saba mchana mazishi yatafanyika huko Pemba na maazishi hayo
yataongozwa na Viongozi wa serikali, Wabunge na CUF.
Mtatiro amewaomba wanachama nba wafuasi wa CUF jijini Dar es Salaam
kujitokeza kwa wingi kuuga mwili wa Mbunge huyo aliyefikwa na umauti akiwa
kazini katika vikao vya Kamati za Bunge, ambapo Marehemu alikuwa Mjumbe wa
Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
No comments:
Post a Comment