March 28, 2013

WANAJESHI WA RWANDA(JUR) WAFANYA ZIARA YA KIMAFUNZO WIZARA YA NISHATI NA MADINI


Wanafunzi wa Kozi ya Ukamanda na Unadhimu kutoka Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) walipotembelea Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kupata maelezo kuhusu vyanzo vya nishati nchini na changamoto zake. Wizara ya Nishati na Madini kupitia Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Hosea Mbise, imesisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya Tanzania na Rwanda katika masuala ya nishati.

Kamishna wa Nishati na Masuala ya Petroli, Mhandisi Hosea Mbise, akipokea zawadi kutoka kwa Makamnda hao Wanafunzi wa Jeshi la Rwanda.


Makamanda hao Wanafunzi kutoka Jeshi la Ulinzi la Rwanda wakisikiliza na kufuatilia kwa umakini maelezo kutoka kwa Kamishna wa Nishani na Masuala ya Petroli.

No comments:

Post a Comment