Baadhi ya Maofisa wa Ofisi Ndogo ya Bunge,wakimsaidia kwa kumbeba
Mbunge wa Chambani,Bwa.Salim Hemed Khamis,mara
baada ya kuanguka ghafla hapo jana jijini Dar akiwa katika vikao vya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kukimbizwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
kwa matibabu ya haraka.
Endelea kufuatilia Father Kidevu
Blog, taarifa zaidi.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema Peponi-Amin
*****
*********
Mbunge wa Chambani-Pemba, Kisiwani Zanzibar Salim Hemed Khamis ambaye jana
aliugua ghafla wakati wa Kikao cha Kamati ya Bunge ya Mambo ya nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, ofisi ndogo jijini Dar es Salaam Amefariki.
Khamis,mara baada ya kugua ghafla
alisaidiwa na Wabunge wenzake na Maofisa wa Bunge na kukimbizwa Hospitali ya
Taifa Muhimbili, kwa matibabu na mchana huu amefariki dunia.
Taratibu za kuusafirisha mwili wa
Marehemu kuelekea Pemba kwa mazishi zinafanyika.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema Peponi-Amin
No comments:
Post a Comment