Tarehe 20 mwezi Machi katika kipindi cha
televisheni cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE kinachorushwa na vituo vya
televisheni vya ITV na Clouds TV kila Jumatano ikiwa ni Sehemu ya pili
kati ya mfululizo vipindi hivyo halisia, Watanzania Daniel Msekwa na
Mwalimu Akida Hamad walionyesha namna ambavyo mtu hapaswi kukata tamaa baada
ya kushinda kwa kuwatoa wapinzani wao kutoka Kenya na Uganda katika raundi ya
kwanza na kutinga nusu fainali, hatimaye
kujinyakulia Dola za kimarekani 5,500 katika ukuta wa GUINNESS.
Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad
wameonyesha namna gani kama mwanamichezo hapaswi kukata tamaa uwapo uwanjani na
wanamatumaini makubwa kuwakilisha nchi katika mashindano ya Pan African ambapo
wanaweza kushinda hadi dola za kimarekani 250,000.
Washiriki bora watakwenda kukutana ana
kwa ana na mashabiki wa soka kutoka nchi za Cameroon,Ghana,Kenya, na Uganda ili atakayeonyesha ujuzi zaidi atavishwa taji
la ubingwa wa` Pan-African’ na kupata kitika cha fedha kitakachobadilisha
maisha yao.
Washiriki wote wana nafasi
kuonyesha ujasiriwa kuipigania nchi yao.
GUINNESS ilizunguka katika nchi yetu kusaka washiriki wazuri watakaonyesha
umahiri wao wakiwa na matumaini lukuki na timu itakayoonyesha ujuzi zaidi
itachaguliwa katika hatua nyingine ya kipindi hiki cha msimu wa pili.
Katika Episodi ya pili ya mashindano haya
yatakayooneshwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne ndizo
zitakua uwanjani kuchuana vikali, ni timu ipi itakayowapiga chini wengine na
kuingia katika hatua ya Pan Africa? Majibu yote yatapatikana siku ya Jumatano.
Hizi ndizo timu zitakazochuana vikali
katika kipindi cha pili wiki hii cha GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE kinachorushwa
na televisheni za ITV na Clouds TV.
Blue team –
Tanzania – Magpies:
Simon
Chimbo(21), Emmanuel Temu(20), wote kutoka Dar Es Salaam, ni mashabiki
wakubwa wa Manchester United. Simon anasoma Teknolojia ya mawasiliano
katika chuo cha Utawala wa Fedha IFM na Emanuel ni mcheza
soka kutoka timu ya Mt. Camlius.
Red team –
Kenya – Hawks:
Wawili
hawa wanatoka Mombasa watavaa mashati mekundu kuonyesha upendo wao kwa mpira wa
miguu katika sehemu ya pili Nyuma Donald Otieno( 36), atakuwa nguzo ya timu
,Awadh Mbarak(22), ataangalia masuala fiziki. Donald ni mwalimu wa soka
na Awadh ni mwanafunzi
Green team –
Uganda – Flex:
Mfanyabiashara Ibra Kawooya, (30),
kutoka Namusuba na mwenzie Alex
Muyobo(31) ambaye alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya mguu, wote ni mashabiki wa Manchester United .
Black team –
Kenya – The Blues:
Francis Ngigi (23), kutoka
Nairobi na Kepha Kimani (25), kutoka Thika watakaovalia fulana nyeusi
watawakilisha Kenya katika sehemu ya 2. Francis ni Mfanyabiashara
na ndo anatarajiwa kuwa kichwa cha Timu.
Wapenzi
wa kipindi hiki cha Guinness Football Challenge barani Afrika wanakumbushwa
kwamba, wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com.
Pia GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE ina
kurasa ya Facebook ambayo ni www.facebook.com/guinnesskenya Ili kufuatilia kwa karibu yanayojiri,
unatakiwa kufatilia ukurasa huu yaani
‘like’ na utakuwa unapata habari zote zinazohusu mchezo huu.
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi
cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki
katika runinga yako.
Usisahau pia kuwa na chupa ya bia
uipendayo ya Guiness wakati unaangalia
kipindi hiki.
*Haiuzwi kwa walio na Umri
chini ya miaka kumi na nane. Tafadhali
Kunywa kistarabu.
No comments:
Post a Comment