March 28, 2013

PRF. J, MR NICE KUPAMBA TAMASHA LA BADILISHA UGANDA



Wasanii wa Tanzania, Joseph Haule ‘Prof. J’ pamoja na Nice Mkenda ‘Mr Nice ni miongoni mwa wasanii kadha wa Afrika Mashariki ambao watapamba tamasha la badilisha live nchini Uganda.



Tamasha hilo kubwa la burudani linaloratibiwa na Mwanamuziki wa Bongo Fleva wa nchini humo Dk. Jose Chameleone linataraji kufanyika Aprili 26, mwaka huu katika viwanja vya Rugby vya Kyadondo.



Akizungumzia Tamasha hilo Chameleone katika moja ya kurasa zake za Facebook na Twitter, amesema mambo yanaebnda poa na Wasanii kibao wamethibitisha kushiriki tamasha hilo.



Mbali na Prof. J na Mr Nice kutoka Tanzania, wengine ni  Redsan kutoka Kenya, Massamba  wa nchini Rwanda.

No comments:

Post a Comment