Na James
Gashumba, EANA
Jukwaa la
Afya la Afrika Mashariki (EAHP), taasisi inayolenga kuwezesha na kuboresha
sekta ya afya, ilizinduliwa juzi mjini Kigali, Rwanda huku wito ukitolewa kwa
serikali za kanda hiyo kushirikiana na taasisi hiyo kwa manufaa ya jamii.
EAHP pia
inalenga kuleta maendeleo katika katika taasisi za afya na kuoanisha sera na
sheria zinazohusiana na sekta ya afya katika kanda hiyo ya Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa Shirika Huru la
Habari la Afrika Mashariki (EANA)jukumu la taasisi hiyo pia ni pamoja na kutoa
msukumo kwa sekta binafsi na asasi za kiraia juu ya masuala ya afya na
wataalamu wamasia kutoka nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Akizindua taasisi hiyo, Naibu
Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia Tija na Sekta ya Jamii, Jessica Eriyo
alisema juhudi hizo zitasaidia kuboresha sekta ya afya katika kanda.
''Tunahitaji watu wenye afya
na wazalishaji ambao wananufaika na ubora na unafuu wa huduma za afya katika
kanda.Hii tu si kwamba inaendana na mkakati wa EAC lakini pia inaendana na
mikakati ya sasa ya maendeleo ya Afrika Mashariki,'' alisema.
Alisisitiza umuhimu wa
serikali kushirikiana na sekta binafsi kuunga mkono juhudi hizo ili
kushughulikia changamoto zinazoikabili sekta ya afya.
Eriyo alitoa wito wa kuwepo
kwa kampeni zaidi kuelimisha wananchi juu ya masuala ya afya katika
ngazi za chini kabisa ambako asilimia 70 ya magonjwa yanayowasumbua raia
yanaweza kuzuilika.
Mwenyekiti wa EAHP, Dk Amit
Thakker pia alibainisha kwamba watu wengi bado wanaugua magonjwa ambayo
yanaweza kuzuilika.
''Tunataka kuzindua kwanza
jukwaa hili na halafu tuone kitakachofuata katika kushughulikia changamaoto
zinazoikabili sekta hii kwa kupeana taarifa na kufanyakazi kwa pamoja katika
,'' alisema Thakker.
No comments:
Post a Comment