Kiongozi wa Tip Top connection Bwana Madee moja
ya kikundi kitakachotumbuiza katika Matamasha ya Airtel Yatosha akiongea wakati
wa uzinduzi wa Matamasha hayo yaliyofanyika katika ofisi za Airtel morocco,
Matamasha haya yatawashirikisha wasanii wengine wakiwemo Fid Q,
Juma Nature, Ney wa Mitego na Stamina.Kulia Meneja Mauzo Airtel
Kanda ya Pwani Raphael Daudi
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando
akiongea wakati akitangaza wa Airtel wa kufany Matamasha ya Airtel Yatosha
katika mikoa mbalimbali ya Tanzania yenye lengo lan kutoa burudani sambamba na
kuelimisha Jamii na wateja wake kuhusu huduma za Airtel ikiwemo
kuitambulisha huduma mpya ya Airtel Yatosha. Kulia Meneja Mauzo Airtel
Kanda ya Pwani Raphael Daudi
*****
******
Airtel Tanzania leo imetangaza mpango wake wa kufanya
matamasha ya Airtel Yatosha yenye lengo la kutoa burudani na kuwaelimisha jamii
na wateja wake juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Airtel ikiwemo
huduma mpya Airtel Yatosha inayomuwezesha mteja kupiga simu kwenda mtandao
wowote kwa gharama nafuu zaidi.
Akiongea wakati wa kutambulisha matamasha hayo, meneja
uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema “Airtel tumeamua kutoa
burudani wakati wa msimu huu wa sikukuu ikiwa ni pamoja na kuitambulisha huduma
yetu ya Airtel yatosha kwa watanzania, tunaamini kwa kupitia matamasha
yatakayofanyika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania wateja wetu na watanzania
kwa ujumla watapata burudani na kupata nafasi ya kupata elimu juu ya huduma
zetu Nyingi
“Safari yetu ya burudani za Airtel yatosha itaanza
katika Mkoa wa Morogoro katika siku ya Jumapili na Jumatatu ya Tarehe
31/3 na 01/04/2013, Kuanzia Saa Tatu kamili Asubuhi mpaka saa Kumi na
Mbili Jioni, pale katika viwanja vya Sabasaba.
Tutakuwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Fid
Q, Juma Nature, Ney wa Mitego na Tip Top
Connection. Kiingilio ni BURE , tunapenda kukukualika wewe na washikaji zako
wote kuhudhuria katika tamasha hili la kwanza kabisa pale morogoro na utape
burudani kabambe. Njoo na Kitambulisho chako ili uunganishwe na ufurahie ofa
nyingi toka Airtel” aliongeza Mmbando .
Naye kiongozi wa Tip Top connection Bwana Madee
alisema” kama kawaida tumejipanga kuwapa wateja wa Airtel na watanzania
burudani ya Ukweli katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, tunaomba watanzania
wajitokeze kwa wingi katika matamasha haya ya Airtel Yatosha. Mbali na sisi
kutoa burudani itakuwa nafasi pia kwetu kuona vipaji mbalimbali vya mashabiki
wetu ambao ndio wasanii nyota wa kesho hivyo tuwapa hamasa ya kujitokeza kwa
wingi ili tuweze kuburudika pamoja.
Wasanii watakaoshiriki katika Matamasha maalumu ya
Airtel yatosha watatumbuiza kwa vibao vyao mahiri kama vile Fid Q na kibao
chake cha Sihitaji Marafiki na Ney wa Mitego na kibao chake cha Nasema
Nao huku Tip Top Connection wakiwakilisha na kibao chao cha Nani kamwaga pombe
yangu.
Airtel hivi karibuni imezindua huduma ya Airtel
Yatosha inayomuwezesha mtumiaji wa mtandao wa Airtel kupiga simu kwenda
mitandao yote kwa gharama ya chini kabisa na hivyo kutokuwa na haja tena ya
kubadilisha kadi ya simu pindi anapohitaji kuongea na mtu wa mtandao
mwingine. Mteja anajiunga kwenye huduma hii kwa kupiga *149*99#
No comments:
Post a Comment