March 28, 2013

WAKENYA WAFURUKUTA GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE

Mmoja wa waendesha kipindi cha Guinness Football Challenge Larry Asago.

Jana usiku  kupitia televisheni  za ITV na Clouds TV mashindano ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ yalituonesha ni kwanini ushirikiano ni muhimu kwa  washiriki kuonyesha ujuzi wao. Francis Ngigi and Kepha Kimani kutoka Kenya walifanikiwa kuingia hatua ya mwisho  na kujipatia fedha za kimarekani  dola 3,000 shukrani kwa vipaji vyao na ushirikiano mzuri.



Francis na Kepha wana nafasi ya kuiwakilisha nchi yao katika mashindano yajayo ya Pan-African ambapo wanaweza kubahatika kujinyakulia  kitita cha fedha  za kimarekani hadi kufikia dola  250,000. Katika kipindi kijacho cha mashindano haya kinachorushwa na vituo vya televisheni vya ITV na Clouds TV, timu nne mpya zitaingia uwanjani kupambana vikali ili kujua ni nani ataibuka mshindi  na kutambulika kama wachezaji na si tu mashabiki,watatakiwa kushinda na kuziwakilisha nchi zao katika mashindano ya Pan-African.



GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya  Endemol.  Kipindi hiki kinarushwa kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV.  Kipindi kitaruhswa na kituo cha ITV kuanzia saa tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku  ambapo  Clouds TV itarusha kipindi hicho  saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku .



Tafadhali kunywa kistaarabu - Hairuhusiwi kwa wenye umri chini ya miaka 18.

No comments:

Post a Comment