Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kudhibiti Matumizi ya Tumbaku Nchini
(Tanzania Tobacco Control Forum), Lutgard Kagaruki akizindua filamu ya The
sixth commandment jijini Dar es Salaam Jumapili iliyopita. Katikati mwenye nguo
nyeupe ni Mkurugenzi wa wa Simbeye Film Company na baadhi ya wasanii
walioshiriki kucheza filamu hiyo.
*****
Jina: The sixth commandment
au Amri ya sita
Muongozaji: Finnigan wa
Simbeye
Urefu: Part I na II jumla
masaa 3
Maelezo: Filamu ya The
sixth commandment au Amri ya sita inamhusisha msichana mdogo, Catherine Sinda
anayecheza kama Maua, binti wa kiongozi wa kanisa ya Yahweh (Mungu) Aliye Juu,
Bishop Msemakweli Mkali.
Bishop Mkali nafasi
inayochezwa na Finnigan wa Simbeye, mwandishi wa biashara wa gazeti la Daily
News, ni kiongozi madhubuti ambaye anaiongoza familia yake kwa umakini mkubwa
kama familia ya mfano kufuata matakwa ya Mungu kama ilivyo kwenye maandiko
matakatifu ndani ya Biblia.
Maua ambaye ni mwimbaji
katika kwaya ya vijana katika kanisa linaloongozwa na baba yake, anapata virusi
vya Ukimwi kwa bahati mbaya wakati akimuhudumia rafiki yake, Mrs Poa ambaye ni
mke wa Mchungaji Babalao Poa msaidizi wa Bishop Mkali kanisani.
Mrs Poa aliumia wakati
akitoka dukani kununua vinywaji kwaajili ya ugeni wa wanakwaya wenzake na Maua
waliokuja nyumbani kumuona Pastor Poa ambaye ni mlezi wa kwaya ya vijana ya
kanisa la Yahweh.
Akijaribu kumhudumia Mrs
Poa, Maua anajisahau kwamba naye ana kidonda kibichi alichoumia siku chache tu
wakati akikata viungo, na kwahiyo kuruhusu damu ya rafiki yake igusane na yake.
Kwa Bishop Mkali kila
aliyeathirika na Ukimwi ni mzinzi ambaye adhabu yake stahiki ni kifo na kwahiyo
Maua anastahiri adhabu hiyo kwa kukiuka mafundisho ya Biblia na familia yake.
Maua anashindwa kuhimili manyanyaso ya baba yake huyo na kuamua kujiua kwa
kumeza vidonge.
No comments:
Post a Comment