Rais wa Jamhuri yaKidemokrasia ya Congo( DRC)
Joseph Kabila (kushoto) akipokelewa na Waziri wa Uvuvi Dkt. David Mathayo
Dec,7,2012 katika uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Jk . Nyerere jijini Dar es salaam
Rais Yoweri Museveni wa Uganda (kulia) akisalimiana
na Makamu wa Rais wa Tanzania Dr. Gharib
Bilal (kushoto) Dec,7,2012 alipowasili katika Uwanja wa ndege
wa kimataifa wa JK ,Nyerere jijini Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa
dharura wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Rais wa Mozambique Armando Guebuza (kushoto)
akipokelewa na Waziri wa Mambo ya nchi za nnje na ushirikiano wa kimataifa
Bernard Membe (kulia) kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK , Nyerere
jjijini Dar es Salaa- Dec,7,2012 kuhudhuria mkutano wa SADC
Makamu wa Rais wa Zambia Dkt.Guy Scott (kulia) akifurahia jambo
na Waziri wa Uchukuzi Dkt, Harison Mwakyembe (dec,7,2012) wakati wa mapokezi
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
JK Nyerere jijini DSM kwaajili ya kuhudhuria mkutano wa dharura wa SADC.
Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji Shamim
Nyanduga (kulia) akibadilishna mawazo na baadhi ya Mabalozi wenzake na maafisa
wanaohudhuria mkutano wa dharura wa SADC,walipokutana katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa JK, Nyerere Dec, 7, 2012.
Kikundi cha sanaa ya matarumbeta kinachoongozwa
na gwiji wake Mzee Hoza,kikitoa burudani katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
JK, Nyerere Dec,7,2012 wakati wa mapogezi ya Marais na wajumbe mbalimbali
wanaohudhuria mkutano wa SADC jijini Dar Es Salaam. (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
No comments:
Post a Comment