Amiri
Jeshi mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Uhuri akiwa kwenye gari maalum
la Kijeshi na Sambamba na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali
Davis Mwamunyange walipokuwa wakioa salamu kwa wananchi na wageni mbali
mbali waliofika Uwanjani hapo kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 51
Uhuru wa Tanzania Bara.Kauli Mbiu ya Maadhimisho ya Mwaka huu ni
“Uwajibikaji, Uadilifu na Uzalendo ni nguzo ya Maendeleo ya Taifa letu”.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na usalaama katika
maadhimisho Miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania Bara,leo katika Uwanja wa
Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Brass Band cha majeshi ya Ulinzi na usalama kikitumbuiza katika maadhimisho hayo.
Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakipokea salamu
za heshima kutoka kwa Vikosi mbali mbali vya Ulinzi la Usalama wakati wa
maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika leo
kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Viongozi
mbalimbali wakiwa katika maadhimisha hayo,kutoka kulia ni Rais wa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Mh. Joseph Kabila,Mama Maria Nyerere,
Rais wa Msumbiji,Mh. Armando Guebuza,Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal na Rais Mstaafu wa awamu
ya pili,Mzee Ali Hassan Mwinyi.
Makamu
wa Rais Dkt.Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Mama Fatma Karume mara
baada ya kuwasili uwanjani hapo.katikati ni Waziri Mkuu,Mh. Mizengo
Pinda.
Vijana wa chipukizi wakionyesha michezo na ujumbe mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo.
Kikosi
cha wanaanga cha Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikitoa salamu za
heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jakmhuri ya Muungano ya
Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kikosi
cha ardhini Jeshi la wananchi la Tanzania (JWTZ) kikitoa salamu za
heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jakmhuri ya Muungano ya
Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Vikosi
vya Ulinzi na Usalama vikiwa vimejipanga tayari kwa gwaride la utii na
heshima mbele ya Amiri jeshi Mkuu na Rais Jamhuri ya muungano ya
Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.Picha kwa hisani kubwa ya Full
Shangwe Blog.
No comments:
Post a Comment