December 18, 2012

SAJUKI ALIPOANGUKA JUKWAANI ARUSHA


MWINGIZAJI wa filamu nchini, Sajuki alidondoka jukwaani juzi wakati akijaribu kuwasalimia mashabiki wake waliofurika kumtazama kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Sajuki  ambaye jina lake halisi ni Juma Said Kilowoko alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kupungukiwa dawa na kulazimika kwenda kutibiwa nchini India.
Mwingizaji huyo alipanda jukwaani katika tamasha la lililowahusisha wasanii wa filamu na muziki, lakini ndoto yake ya kusalimia mashabiki wake hakuwezekana. 

 Mara baada ya kukabidhiwa kipaza sauti Sajuki alitamka neno moja ”ahhh" na kudondoka chini na wasanii wenzake walimsaidia kuinuka na kumuondoa jukwaani hapo. Akizungumza na gazeti hili muda mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki alisema hali yangu si nzuri kwani nahishiwa nguvu na anahitaji matibabu zaidi.

”Kaka hali yangu si nzuri kabisa naumwa, sijisikii vizuri,” alisema Sajuki huku akionekana mnyonge zaidi
Hata hivyo, mashabiki wamefurika uwanjani hapo walionyeshwa kustushwa na hali hiyo na kushutumu wasanii walioamua kumtumia ili wapate fedha ihali mwenzao ni mgonjwa.

“Hawa watu wa Bongo movie ni watu wa ajabu huyu mtu anaumwa, badala ya kumwacha apumzike wenyewe wanamzungusha bila ya kujali afya yake,” walisema mashabiki hao.

No comments:

Post a Comment