December 13, 2012

REDDS MISS TANZANIA 2012 AWASILI MKOANI KAGERA


Redds Miss Tanzania 2012, Brigitt Alfred amewasili jana Mjini Bukoba kwaajili ya ziara ya kutembelea vituo mbalimbali vya watoto yatima, na baadae ataenda jijini Mwanza kwa shughuli kama hizo za kusaidia jamii.
Redds Miss Tanzania 2012, Brigitt Alfred akiwa katika picha ya pamoja na matron wake Irene Karugaba mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba, kushoto ni mkuu wa itifaki wa kamati ya maandalizi ya Miss Tanzania, Alfred Makoye.
 Redds Miss Tanzania 2012, Brigitt Alfred, Akiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya kimataifa ya Victorious Perch iliyoko katika manispaa ya Bukoba wa tatu toka kushoto ni Audax Mutiganzi mmoja wa wamiliki wa mitandao ya kijamii.

Miss Redds Tanzania 2012 akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa hoteli ya victorious, Kulia ni Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Maandalizi ya Miss Tanzania, Alfred Makoye na kushoto ni matron wa Miss huyo Irene Kalugaba.

No comments:

Post a Comment