Fainali
za kumsaka Unique model of the year 2012 katika shindano la Unique model
zitafanyika katika tarehe 28 desemba mwaka huu katika ukumbi wa New Maisha club
uliopo Oyterbay jijini Dar.
Fainali hizi zitasindikizwa na burudani ya toka bendi ya
Mashujaa ikiongozwa na Chaz Baba,mfalme Costa Siboka atatoa burudani ya vionjo
vya nyimbo za asili na upande wa bongo flava kutakuwa na suprize yakufa mtu,pia
kwa mara kwanza jukwaani msanii Bshop atapiga bonge la shoo.
Wapenzi wa burudani na tasnia ya mitindo wameombwa
kujitokeza kwa wingi kushuhudia nani atavishwa taji hilo ambalo limekua gumzo
jijini Dar kutokana na ushindani mkubwa kati ya washiki hao 12.
Red carpet kwa mastaa na watu wote watakaopendeza siku
hiyo itakuepo,pia kutakua na kitu kipya kabisa katika matukio ya mitindo
nchini Tnzania.
Baada ya shindano kumalizika burudani ya wasanii kibao wa
bongo flava itaendelea mpaka alfajiri kwani tumepania kukonga nyoyo za
mashabiki wa burudani siku hiyo ambapo uhondo huo wote utakuwa ni kwa Tsh
15,000/= tu.
No comments:
Post a Comment