Rais
wa zamani wa Madagascar Marc Ravalomanana akifafanua jambo wakati wa
mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam leo December
11, 2012,kulia ni Mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa zamani wa Madagascar Marc Ravalomanana
wakati wa mkutano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam leo
December 11, 2012.PICHA NA IKULU
********
Na Veronica Kazimoto – MAELEZO
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete
amefanikiwa kufanya mazungumzo na Rais wa zamani wa Madagaska Marc Ravalomanana
ambaye amekubari kurudi nchini kwake baada ya kuwa uhamishoni nchini
Afrika Kusini tangu mwaka 2009.
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam
leo, Raisi Kikwete amesema Ravalomanana
amekubali pia kutokugombea katika uchanguzi utakaofanyika nchini humo mwezi Mei
2013 ili kuleta amani na utulivu.
“Nimezungumza na Rais Ravalomanana na amekubali kurudi nchini
kwake madagaska na kukubali kutokukugombea
uchaguzi ujao kama maamuzi ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) yalivyofikiwa katika vikao vyake vya
hivi karibuni”, amesisitiza Rais Kikwete.
Raisi kikwete amefafanua kuwa Ravalomanana anarudi nchini Madagaska bila masharti yoyote
na atapewa ulizi na Serikali ya nchi hiyo ikisaidiana na Jumuiya ya SADC. Kwa upande wake Rais Ravalomanana amemshukuru
Rais kikwete kwa kufanikisha mazungumzo hayo
na amesema anaheshimu maamuzi
yaliyotolewa na SADC kwa lengo la kuisaidia Madagaska kuwa katika hali ya
amani.
“Ninamshukuru Rais Kikwete kwa
kufanikisha mazungumzo haya na niko tayari kurudi nchini kwangu kujenga,
kuimarisha na kushirikiana na wananachi
ili kuleta amani na utulivu,” amesema
Ravalomanana.
Rais kikwete alipewa jukumu na Jumuiya
ya Maendeleo ya Nchi
za
Kusini mwa Afrika la kufanya mazungumzo
na Marais wote wa wawili, Rais wa sasa wa
Madagaska Andry
Rajoelina na Rais wa zamani Marc Ravalomanana ambapo mazungumzo bado
yanaendelea kwa upande wa Rais Rajoelina.ezi Mei

yanaendelea kwa upande wa Rais Rajoelina.
No comments:
Post a Comment